HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 22, 2018

MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itawasomea maelezo ya awali (PH) na kesi kuanza kuisikiliza kesi ya jinai inayowakabili viongozi wa juu wa tisa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kwa mfululizo kuanzia Juni 25 hadi 29 mwaka 2018.

Hati hiyo imekuja baada ya mawakili wa upande wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili Paul Kadushi, Wankyo Simon na Jackline Nyantori kuieleza mahakama kuwa, kesi ilikuja kwa ajili ya Ph .

Hata hivyo, Mahakama haikuweza kusoma PH kwa sababu mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Freeman Mbowe amefiwa na kaka yake na amesafiri jana kwenda kuzika Moshi.

Pia Mahakama imemtaka mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo, Mbunge wa Tarime mjini Estherher Matiko ambaye amekuwa akiripotiwa kuwa mgonjwa mara kadhaa, kuhudhuria mahakamani bila ya kukosa na asipofanya hivyo hatua dhidi yake zitachukuliwa.

Pia kesi hiyo imeshindwa kuendelea kusikilizwa ysikilizwaji wa PH leo sababu mawakili wanaowatetea washtakiwa hao Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya hawakuwepo walikuwa na kesi zingine, Kibatala ana kesi mahakama kuu. Huku Mtobesy alikuwa amehudhuria kesi Mahakama ya Afrika Mashariki Arusha na wamewakilishwa mahakamani hapo na mawakili Nashon Nkungu, Frederick Kihwelo na Hekima Mwesigwa.

Mbowe aliwakakilishwa mahakamani hapo na mdhamini wake Grayson Celestine ambaye aliwasilisha nakala ya cheti cha kifo mahakamani ili kuithibitishia mahakama, huku akiwasilishwa na mdhamini wake Patrick John ambaye alidai Matiko bado anaumwa na akawasilisha nyaraka ya mapumziko kutoka kituo cha afya ambayo inamapumziko ya siku saba kuanzia juni 21,2018 mpaka Juni 28,2018.

Hata hivyo nyaraka hiyo ilipingwa na Wakili Nchimbi kwa madai kuwa ni batili haina maelezo yanayojitosheleza ambayo yanaweza kuishawishi mahakama kuamini Matiko ni mgonjwa na anapaswa kupumzika kwa siku saba.

Nchimbi alidai awali Matiko alikwisha wasilisha nyaraka kama hiyo ambayo ilimpa mapumziko ambayo yalipaswa kuisha Juni 23,2018 ambayo ilitlewa na kituo hicho kimoja cha afya

Alidai katika mazingira ya kawaida kuwepo kwa mkanganyiko huo siyo kitu cha kawaida hivyo aliomba mahakama itoe amri.

Mbali na Mbowe na Matiko washtakiwa wengine ni mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

Katibu wa chama hicho Dk.Vicenti Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Katika kesi hiyo, washtakiwa pamoja na wenzao ambao hawapo mahakamani walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko kutawanyika.

Pia imedaiwa, siku hiyo katika viwanja vya buibui na Mwananyamala wilaya ya Kinondoni washtakiwa hao wakiwa wamekusanyika na azma ya pamoja, waliitekeleza azma yao kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope kuwa watakwenda kupelekea uvunjïfu wa amani.

Pia watuhumiwa hao wanadaiwa kutekeleza mkusanyiko ama maandamano yasiyo halali wakiwa na lengo la kuvamia ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kuĺeta hofu ya uvunjifu wa amani.

Wakili Nchimbi alidai watuhumiwa hao walikaidi tamko lililowataka kutawanyika lililotolewa na afisa wa polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani uliosababisha hofu na hatimaye kifo cha Akwilina na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.

Mbowe anadaiwa, wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo la Kinondoni katika mkutano wa adhara alihamasisha chuki isivyohalali kwa kutoa matamshi yalikuwa na lengo la kuamsha hisia za chuki miongoni mwa watanzania.

Pia Mbowe anadaiwa kutamka maneno mabaya yaliyokuwa na nia ya kuinua hali ya kutoridhika miongoni mwa watanzania dhidi ya serikali halali iliyopo madarakani

Mshtakiwa Mdee anadaiwa kutamka maneno yaliyokuwa na lengo kuhamasisha hisia za chuki miongoni mwa watanzania.

Kwa upande wa Heche anadaiwa kutamka maneno yaliyokuwa na lengo kuamsha hali ya kutoridhika miongoni mwa watanzania dhidi ya utawala uĺiopo madarakani.

Mbowe pia anadaiwa kutoa maneno yaliyokuwa na na nia ya kuleta chuki na hali ya manung'uniko miongoni mwa jamii dhidi ya utawala ulïopo madarakani.

Pia anadaiwa kutoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau kwa upande wa raia wa Tanzania dhidi ya mamlaka halali kuwa "Hii nchi

Aidha anadaiwa kuwashawishi wakazi wa Kinondoni kutenda kosa la kufanya maandamano na mkusanyiko usio halali.

Mshtakiwa Msigwa anadaiwa kushawishi Raia na wakazi wa eneo hilo kutenda kosa la jinai kwa kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha

Aidha, Bulaya anadaiwa kutenda kosa la kukaidi amri halali ya tamko.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad