HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 16 June 2018

KIKUNDI CHA BEAUTY WITH BRAIN,SERENA HOTEL WAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KURASINI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Katika kuadhimisha  ya siku ya mtoto wa Afrika leo kikundi cha Beauty with Brain kwa kushirikiana naSerena Hotel  wamemtoa msaada wa vitu mbalimbali kwa kituo cha watoto wanaoishi  kwenye mazingira cha serikali kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam. 

Beauty with Brain pamoja na Serena waliweza kukabidhi vyakula, mafuta ya kupikia, masweta ya watoto, rangi na gypsum kwa ajili ya ukarabati wa sehemu ya kulia chakula, vitabu, nguo na baadhi ya vitu vingine.

Akizungumza ma wanahabari baada ya kukabidhi kwa vitu hivyo, Mwenyekiti wa Beauty With Brain Teddy Mapunda alisema kuwa lengo kuu la kuwasaidia watoto hao ni kuwafanya wajisikie wanafamilia zinazowapend√†  na kuwajali pia.

Teddy amesema, katika siku ya leo wamekuja na zawadi mbalimbali kwa watoto hao ikiwemo vitabi vya kujisomea, masweta 71 kwa watoto wote na pia  nguo na viatu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.

Kikundi hicho kimeweza kushirikiana bega kwa bega na Serena Hotel na kufanikisha kupatiwa kwa zawadi hizo kwa watoto hao ambapo Mkurugenzi wa Rasilimali Wa Serena Hotel Sophia Mketo amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu wameamua kujumuika pamoja na watoto wa kituo cha Kurasini na wameona wanahitaji sana mchango wao.

Sophia alisema wamekuja na makopo ya rangi, gypsum kwa ajili ya kukarabati jengo la kula chakula pia wamekuja na vyakula mbalimbali pamoja na mafuta kwa ajili ya kupikia.

Na  kwa upande wa msimamizi wa kituo cha Kurasini Beatrice Mgumiro amewashukuru Serena Hotel na Beauty with Brain kwa moyo waliouonesha wa kuwakumbuka watoto hao na kuwataka wasiache kuja tena na tena huku akiwaomba wadau wengine wajitokeze ili kuweza kuwasadia watoto hawa.

Kituo cha Kurasini ni kituo cha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu kilichopo chini ya serikali na kimekuwa kinahitaji mahitaji mbalimbali kwa ajili ya watoto hao ambapo Beauty with Brain na Serena Hotel kwa pamoja wameamua kuwakumbuka watoto hao.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja wa wanawake cha Beauty with Brain cha jijini Dar es Salaam,Teddy Mapunda (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitabu mmoja kati ya watoto wanaolelewa katika Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Serikali kilichopo Kurasini,jijini Dar es Salaam,wakati kinamama hao kwa kushirikiana na Hoteli ya Serena, walipotembelea kituo hicho leo asubuhi na kukabidhi Vyakula, Ndoo za rangi, Gipsum Board, Masweta ya watoto wote 71, nguo na viatu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Picha Zote na Nasma Mafoto
Mazungumzo kabla ya kukabidhi msaada huo
Kina mama wa Beauty With Brain wakikabidhi sehemu ya msaada huo kwa watoto wa kituo chaWatoto Yatima ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja wa wanawake cha Beauty with Brain cha jijini Dar es Salaam,Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima Kurasini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Hoteli ya Serena, Sophiaakizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima Kurasini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika leo Jijini Dar es Salaam
msimamizi wa Kituo ya Yatima cha Kurasni Beatrice Mgumiro, akiwashukuru kikundi cha Beauty with Brain pamoja Serena Hotel kwa kuwakumbuka watoto hao wanaoishi katika kituo cha watoto yatima Kurasini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hotel  Serena Hotel wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Hoteli ya Serena, Sophia Mketo (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa tina za kuchanganyia rangi, msimamizi wa Kituo ya Yatima cha Kurasni Beatrice Mgumiro, wakati kikundi hicho kilipofika kituoni hapo kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali leo asubihi. Katikati ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Beauty with Brain, Teddy Mapunda aliyeratibu safari hiyo.No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad