HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 11 June 2018

KIFO CHA SAM WA UKWELI NI PIGO KUBWA KWANGU- RIDHIWANI KIKWETE

Na Shushu Joel, Chalinze 
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze  mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na msiba wa msanii wa Bongo fleva Sam wa Ukweli aliyefariki dunia siku za karibuni.

Akizungumza mara baada ya mzishi ya msanii huyo yaliyofanyika wilayani Bagamoyo Ridhiwani alisema kifo cha Sam wa Ukweli kwake ni pigo kubwa  kwani alikuwa akimtumia katika mikutano yake kama mwamasishaji wa watu kujitokeza kwa wingi kupitia nyimbo zake.

"Nimesononeshwa na msiba huu , nimpoteza mtu muhimu sana lakini sina jinsi, kilichobaki ni kumuombea dua tu ili apumzike kwa amani huko aendako,"amesema Ridhiwani.
Aidha amewataka wasanii na watanzania kuonesha umoja,upendo na mshikamano kama ndugu wa baba na mama mmoja ili kusaidiana.

Kwa upande wa moja ya wazee maarufu katika jimbo la Chalinze Abudalla Mzimba amewashukuru wote waliojitokeza katika mazishi ya kijana na msanii aliyekuwa mfano wa kuigwa katika CCM.

Amefafanua muda mwingi alikuwa akifanya kazi ya kuwahamasisha watu kusogea kwenye mikutano ili kusikiliza kile kilichokusudiwa kusemwa na viongozi wetu wa kisiasa.

Pia ameongeza kuwa kifo cha msanii huyo ni fundisho kwa vijana waliobaki kwa kutokusema ukweli magonjwa yanayowasumbua bila kwenda kutafuta tiba katika sehemu husika .

Mazishi ya Sam wa Ukweli yamehudhuliwa pia na Rais msataafu Dk. Jakaya kikwete.
 Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na wasanii wa bongo fleva katika dua ya kumuombea msanii wa bongo fleva alifariki jana na kuzikwa wilayani Bagamoyo.
 Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazishi ya msanii sam wa ukweli.
 Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani kikwete akiteta jambo na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Kikwete kwenye mazishi ya msanii Sam wa ukweli wilayani Bagamoyo.
Rais msaatafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza waombolezaji katika msaba wa msanii wa bongo fleva Sam wa ukweli.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad