HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 30 June 2018

HEALTHY MAISHA YAZUNGUMZIA NAMNA WANAVYOTENGENEZA JUICE

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
KAMPUNI ya Healthy Maisha ambayo imejikita katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya nzuri kwa kula vyakula vyenye lishe imesema pamoja na kutoa ushauri kuhusu vyakula sahihi katika mwili wa binadamu pia wanatengeneza juisi zenye uwezo wa kuondoa sumu mwilini. 

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Kampuni ya Healthy Maisha Amina Mkiko wakati akizungumzia shughuli ambazo zinafanywa na kampuni yao katika kuhakikisha afya za watanzania zinakuwa salama. 

Amesema kuwa kampuni yao imejikta zaidi katika kutoa elimu na ushauri kuhusu chakula sahihi ambacho mtu atakula na afya yake ikabaki salama bila kushambuliwa na magonjwa. 

Ameongeza mbali ya kutoa ushauri wanajihusisha na kutoa ushauri wa chakula gani ambacho mhusika anayekwenda kwao kupata ushauri ale huku pia wakijihusisha na upikaji wa vyakula vyenye mlo kamili. 

“Jukumu letu ni kuhakikisha afya ya kila mtanzania inakuwa salama.Hivyo tunatoa ushauri wa aina ya vyakula na kubwa zaidi baada ya chakula tunawahamasisha wananchi kunywa maziwa ya Asas,’amesema. 

Wakati huo huo amesema wanatengeneza juisi zenye mchanganyiko wa maziwa ya Asas ambapo juisi hiyo kazi yake ni kuondoa sumu mwilini. 

Amesema juisi hiyo hutengenezwa kwa matunda ya aina mbalimbali na wakati wa kuitengeneza hawaweki maji zaidi ya maziwa ya Asas ambayo yamekidhi vuwango vya ubora,”amesema Mkiko. 

Ameongeza wakiwa kwenye maonesho hayo watatoa ushauri kwa wananchi wote ambao wataingia kwenye banda la Asas ambako wako na wamejipanga kwa kutoa huduma.
Meneja wa Kampuni ya Healthy Maisha Amina Mkiko akielezea namna wanavyotengeneza matunda na mbogamboga kwa ajili ya juice za kuondoa sumu mwilini kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa.
Meneja wa Kampuni ya Healthy Maisha Amina Mkiko pamoja na wafanyakazi wenzake wakionyesha matunda mbalimbali na maziwa na ASAS wanayotengenezea juice za kuondoa sumu mwilini. 
Meneja wa Kampuni ya Healthy Maisha Amina Mkiko katikati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake katika banda la Kiwanda cha Maziwa cha ASAS DAIRIERS LTD.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad