HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 14 June 2018

ECOBANK YAPANDA MITI 130 UFUKWE WA BARABARA YA BARACK OBAMA JIJINI DAR

BAADA ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kufungua ukuta uliojengwa katika ufukwe wa barabara ya Barack Obama jijini Dar es salaam, leo June 14 Ecobank wamepanda miti ipatayo 130 ili kutunza  mazingira yanayozunguka eneo hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee ameeleza kuwa benki hiyo ni ya watu na inajali jamii inayowazunguka hivyo suala la mazingira linapewa kipaumbele kwa kiwango cha juu.

Ameeleza kuwa zoezi hilo la upandaji miti linafanywa na nchi 33 Afrika ambazo Ecobank inatoa huduma zake wakiwa na kauli mbiu ya  "Panda leo, Uilinde kesho."

Mwanahiba amesema kuwa kwa Tanzania wameandaa miti 500 katika shule ya awali na msingi iitwayo kisimani iliyoko Arusha na leo wamepanda miti 130 katika fukwe hizo.

Aidha ameeleza kuwa wamejikita katika kubadilisha mfumo wa kibenki wa Afrika katika kuwahudumia wateja kwa ufanisi, rahisi na kwa gharama nafuu kama vile, utumiaji wa aplikasheni ya simu (mobile app) ambayo hadi sasa imepakuliwa na zaidi ya wateja Milioni 5.

Pia amewashukuru wafanyakazi wa Ecobank kwa kwa ushirikiano wao katika kuungana na jamii kwa kuhakikisha watoto na vizazi vijavyo wanafurahia matunda ya utunzaji wa mazingira katika sayari hii adimu.

 Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee(kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Sea View, Victor Angelo Muneni(kulia) wakipanda mti kwenye fukwe ya barabara ya Barack Obama wakati wa hafla ya upandaji miti katika eneo hilo leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee pamoja na Mwenyekiti wa Sea View, Victor Angelo Muneni na Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala Feada Magesa wakimwagilia maji moja ya mti walioupanda wakati wa zoezi wa upandaji miti 130 katika eneo la fukwe ya barabara ya Barack Obama.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank pamoja na wadau wa mazingira wakipanda miti katika eneo la fukwe ya barabara ya Barack Obama wakati wa zoezi la upandaji miti 130 iliyotolewa na benki hiyo. 
   Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti 130 katika eneo la fukwe ya barabara ya Barack Obama. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Furaha Samalu na kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Sea View, Victor Angelo Muneni
Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Afisa Mazingira, mwenyekiti wa Mtaa wa Sea View, wafanyakazi wa Ecobank pamoja na wadau wa mazingira mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti 130 katika eneo la fukwe ya Barabara ya Barack Obama leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad