HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 30 June 2018

Dawa za kulevya zilivyopoteza ndoto yangu ya kuzaa - Leija


Msichana Leija Chawe, muathirika wa dawa za kulevya kwa takribani miaka 15  anasimulia. Kisa kilichomkuta baada ya kutumia dawa za kulevya. Ni katika maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya duniani ambayo nchini Tanzania kitaifa yaliyofanyika Mkoani Iringa.

 Anatokea katika kituo cha kusaidia waathirika wa dawa hizo cha Mtwivila Iringa ( Iringa Sobber House). 

Nilianza kutumia dawa za kulevya nikiwa na umri wa miaka 15 tu, wakati huo nikiwa kidato cha pili.
Nilianza kwa kutumia bangi, nikafuatia Heroine na baadae nikaja kutumia dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Nilijingiza kutumia dawa za kulevya kupitia mwanaune ambaye alikuwa Boyfriend wangu. Nilivuta madawa wakati wa muda wa masomo, baada ya muda wa masomo na kabla ya kulala.

Lakini namshukuru mungu leo ameweza kunisaidia nikasimama mbele za watu, wakati natumia dawa hizi nilikuwa sitambuliki, nilikuwa nanyanyapaliwa, kutengwa, nilikuwa nikiitwa majina mbalimbali kama mteja, changudoa na majina mengine ambayo hayafai katika Jamii.

 Nilikuwa nikilala makaburuni na wakati mwingine nje ya maduka. Nilikuwa nikifanya kazi mbalimbali ambazo hazifai kwa mtoto wa kike, nilikuwa nikizika watoto wachanga wanaofariki mahospitalini, nilichimba makaburi na kukaa makaburini nikisubiri watu wanaokuja kuloga usiku kwa ajili ya kiwazindika mazindiko yao. 

Nilikuwa nikipita sehemu mbalimbali kufanya matukio ya kuiba, kukaba na kufanya vitu vingine ambavyo havifai katika Jamii. Nilitengwa na familia na Mimi pia nilijitenga nayo na Jamii nzima kwa ujumla kwani nilikuwa mchafu, nilikuwa siogi kwa wakati, nilikuwa naoga kwa wiki mara moja saa nyingine ilikuwa inapita mwezi bila kuoga.

Madhara makubwa niliyoyapata kwa kutumia dawa za kulevya ni pamoja na kuharibu kizazi changu na kupoteza kabisa uwezo wa  kuja kuzaa na mimi siku moja kuitwa mama.
Mtoto wa kike unapotumia dawa za kulevya inakufanya usipate hedhi vizuri kila mwezi, hii ilinipelekea kuharibu kizazi changu na kuharibu vitu vingine katika mfumo wangu wa uzazi, lakini namshukuru mungu siku ya leo nimekaa hapa mbele yenu ni mzima na ninaendelea vizuri na ninaishi bila ya kutumia dawa za kulevya.

Nawaasa watoto wa kike wenzangu, mimi sikupenda kutumia dawa  za kulevya ilinitokea kwa sababu ya kufuata mkumbo wa mwanaume nilijikuta nikijiingiza kwenye kuvuta bangi kisha heroine na cocaine, nasikitika sana ninapoona vijana wenzangu hadi sasa wanatumia dawa za kulevya. Nawaambia vijana wenzangu maisha bila ya dawa za kulevya inawezekana,

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad