HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 23 May 2018

WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE

Na Victor  Masangu, Kisarawe
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa  (TAMISEMI)  Selemean Jafo amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya jamii kuwabagua na kuwanyanyasa  makundi ya watu  wenye ulemavu na  badala yake wabadilike na kuwashirikisha kikamilifu katika shughuli zote  za kimaendeleo sambamba na kuwapatia  fursa za ajira katika sekta mbali mbali  ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na kuondokana na wimbi la umasikini.

Jafo ametoa kauli hiyo  wakati wa sherehe za ugawaji wa vifaaa saidizi  kwa watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali wanaotoka katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wadau wa wengine wa maendeleo.

 Katika hatua nyingine  Waziri Jafo alimuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha anawakatia walemavu wote bima ya afya ili waweze kutibiwa bure ili   kuondokana na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata, na kuongeza kuwa atatoa kipaumbele cha kwanza kwa watu  wenye umelamvu katika fursa za ajira zilizotangazwa na serikali.

“Kwa kweli nadhani nyinyi wenyewe mmejionea jinsi ya watu wenye ulemavu wanavyopata tabu, kwa hiyo mimi kiukeli hali hii mimi sijapendezwa nayo na ndio maana nimeshaaznza kuweka mikakati kabambe amabayo kwa hakika itaweza kuwasaidia kwa kisi kikubwa walemavu hawa katika sekta mbali mbali,na kwa sasa ofisi yangu kwa mwaka huu imetoa nafasi za ajira na wao ndio nitawapa kipaumbele cha kwanza katika kupata kazi,”alisema Waziri Jafo.

Kwa upandewake  Mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ummy Nderiananga akizungumza kwa niaba ya wenzake amesema kwa sasa changamoto kubwa ambayo inawakabili ni ukosefu wa kutokuwa na vifaa saidizi ambavyo vinawapa wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku,na kujikuta wanashindwa kuzifikia fursa zilizopo ili kuweza kujikwamua kimaisha.

Pia alitoa pongeza kwa serikali ya awamu ya tano chini ya ofisi ya Waziri kutokana na kuwapa ushirikiano wa kutosha na walemavu katika kuwasaidia vifaa mbali mbali ambayo vimeweza kuwasaidia  walemavu wapatao 695 kutoka maeneo mbali mbali.

 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo aliziagiza halmashauri zote kuhakikisha kwamba majengo ambayo  wanakuwa wanayajengwa miundombinu yake hususan katika vyumba vya madarasa pamoja na vyoo inakuwa ni rafiki,na kutoa wito kwa wawekezaji wa mkoani humo kutoa sapoti ya kuwasaidia walemavu.

VIFAA ambavyo vimetolewa kwa walemavu  hao katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ni pamoja na Baiskeli za miguu mitatu zipatazo 40 viti vya mwendo 15  pamoja na fimbo za kuembelea 100 ambavyo vitaweza kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao  kwa urahisi.
 WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa  (TAMISEMI)  Selemean Jafo (kushoto) akimkabidhi fimbo maalumu kwa ajili ya kutembelea mmoja wa watu wenye ulemavu wa macho, kulia katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa saidizi vikiwemo baiskeli za miguu mitatu zipatazo 40, viti  vya mwendo 15 pamoja na fimbo 100.
  WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa  (TAMISEMI)  Selemean Jafo  (aliyevaa suti nyeusi) akimkabidhi fimbo maalumu kwa ajili ya kutembelea mmoja wa watu wenye ulemavu wa macho,kulia katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa saidizi vikiwemo baiskeli za miguu mitatu zipatazo 40,viti  vya mwendo 15 pamoja na fimbo 100.
  Mwenyekiti wa Shirikisho la wa wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ummy Ndariananga akitoa taarifa kwa mgeni rasmi kuhusina na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali.
  Mkuu wa Wilaya ya  Kisarawe Happiness Seneda akizngumza na walemavu na baadhi ya wananchi ambao walifika katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiuzungumza katika halfa ya ugawaji wa vifaa hivyo kwa watu wenye ulemavu katika  halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.(Picha Na Victor  Masangu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad