HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 11, 2018

WANAFUNZI WA AFYA YA JAMII MUHAS WASHINDA RUZUKU YA UTAFITI WA TB

Na Mwandishi Wetu.

Wanafunzi wawili wa shahada ya uzamili ya Afya ya Jamii wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS wameshinda ruzuku kwa ajili ya kufanyia utafiti kwenye masuala ya Kifua Kikuu, TB Tanzania.

Wanafunzi hao, Lucas Shugulu na Dkt. Calvin Mwasha wamepewa rukuzu ya dola 5000 kila mmoja na shirika la kimataifa lisilo la faida ambalo limejikita katika kupambana na Kifua Kikuu linajulikana kama KNCV Tuberculosis Foundation (KNCV).

Wanafunzi hao wamefanikiwa kupata ruzuku hiyo baada ya kuitikia mwito uliotolewa na KNCV kwa wanafunzi wa uzamili kuwasilisha mapendekezo ya utafiti (research proposals) yatakayojikita kwenye masuala ya kitaifa yanayolenga kifua kikuu. Wanafunzi hawa waliwasilisha mapendekezo yao ya utafiti na kufanikiwa kuchanguliwa kuwa wanufaika wa ruzuku hii ya utafiti kwa mwaka huu. 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Machapisho MUHAS, Dkt Bruno Sunguya amesema utafiti utafiti utakaofanya na hawa wanafunzi utachangia katika masomo yao kwa kuwajengea uwezo wa kuandika andiko la utafiti (Thesis). Dkt. Bruno ameongeza kwamba wanafunzi hawa watasimamiwa wanataaluma wa MUHAS pamoja na wanasayansi wa masuala ya kifua kikuu wa KNCV. They will be co-mentored by faculty at MUHAS and TB scientists in KNCV. 

"Hili ni kundi la pili la wanafunzi wa MUHAS kupata ruzuku ya utafiti ya namna hii. Kundi la kwanza walifanikiwa kutetea vizuri maandiko yao ya utafiti na wamehitimu mafunzo yao mwaka jana, wanafunzi hao pia waliweza kuwasilisha muhtasari wa maandiko yao kwenye makongamano mawili" aliongeza Dkt. Bruno.
 Dkt. Calvin Mwasha akipokea ruzuku aliyoshinda kwa ajili ya kufanya utafiti wa masuala ya kifua kikuu, Tanzania kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa shirika la KNVC, Dkt. Vishnu Mahamba, kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkurugenzi wa Utafiti na Machapisho, MUHAS.
 Mkuu wa Shule ya Afya na Sayansi ya Jamii MUHAS, Dkt. Rose Mpembeni akimpongeza Lucas Shugulu baada ya kukabidhiwa ruzuku aliyoshinda kwa ajili ya kufanya utafiti wa masuala ya kifua kikuu, Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkurugenzi wa Utafiti na Machapisho, MUHAS.
Kutoka kulia ni Mshauri wa Wanafunzi, MUHAS Dkt. Tumaini Nyamuhanga, Mkurugenzi wa Huduma za kiufundi wa Mradi wa Challenge TB, Dkt. Willy Mbawala, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Machapisho MUHAS, Dkt. Bruno Sunguya, Mwakilishi Mkazi wa shirika la KNVC, Dkt. Vishnu Mahamba, Mkuu wa Shule ya Afya na Sayansi ya Jamii MUHAS, Dkt. Rose Mpembeni, mshindi tuzo ya ruzuku ya kufanya utafiti wa TB, Dr. Calvin Mwasha, Mratibu wa digrii ya uzamili ya Afya ya Jamii, MUHAS, Emmy Mehta, mshindi wa tuzo ya ruzuku ya kufanya utafiti wa TB, Lucas Shugulu na Msaidizi wa Ofisi, Joyce Nkta katika picha ya pamoja baada ya tukio fupi la kuwakabidhi hundi washindi wa ruzuku kwa ajili ya kufanyia utafiti kwenye masuala ya Kifua Kikuu, TB Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad