HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 11, 2018

WAKAZI WA KANDA YA ZIWA WAENDELEA KUJIZOLEA ZAWADI ZA MZUKA WA SOKA NA COKA

Promosheni ya Mzuka wa Soka na Coka ya kampuni ya Coca-Cola Nyanza Bottlers ya jijini Mwanza inazidi kuwezesha wateja wa soda kujishindia zawadi ambapo wiki hii wateja 11 wamekabidhiwa pikipiki  na wengine 4 wamekabidhiwa luninga bapa za kisasa.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi,Meneja Masoko na Mauzo wa Nyanza Bottlers,Samwel Makenge ,alisema kumekuwa na ongezeko la washindi ,na kampuni inayo furaha kuona wateja wake wanaendelea kushiriki katika promosheni hii na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali.

“Zipo zawadi nyingi  zimeandaliwa kwa ajili ya wateja wetu zikiwemo pikipiki,luninga bapa za kisasa,fedha taslimu kuanzia 5,000 hadi 100,000/-na soda za bure, tunatoa wito waendelee kushiriki waweze kujishindia”, Alisema Makenge.

Washindi wapatao 15 ambao  walikabidhiwa zawadi zao za Pikipiki naLuninga  katika hafla hiyo iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza, waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuwakwamua wateja wake kiuchumi.
 Meneja Masoko na Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Nyanza, akiongea na waandishi wa habari.
 Washindi mbalimbali wakikabidhiwa zawadi zao.
Baadhi ya washindi wakifurahia zawadi walizojishindia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad