HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 31, 2018

WAKULIMA KUNUFAIKA NA BIMA YA KILIMO KUANZISHA MWAKA HUU- KAMANGA

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

SHIRIKA la bima la Taifa la Tanzania (NIC), limelenga kuanzisha bima ya kilimo mwaka huu, ambayo itasaidia kuwapa usingizi wakulima mbalimbali nchini, waweze kunufaika kwa kujikinga na majanga .

Mkurugenzi mtendaji wa NIC ,Sam Kamanga (pichani), aliweka bayana juu ya mpango huo ,wakati akitolea ufafanuzi masuala ya bima za majanga, wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Alieleza, wamelenga kuanzisha program hiyo wakati wa siku ya wakulima, nanenane na sabasaba mwaka 2018.

"Katika program zetu tunaianzisha program hii ya bima ya kilimo ,kusudi kumpa mkulima nafuu ,kwani ni asilimia 75 ya watanzania wananufaika na kilimo"

"Kukitokea majanga wakulima hao huwa wakipoteza muelekeo ,tunataka kumpa usingizi mlaji ,hata akitokewa na janga shambani ama gari lake limeangukiwa na mti awe anajua atakingwa na kulindwa na bima yake" alifafanua Kamanga.

Akielezea baadhi ya gharama za kukata bima , Kamanga alisema nyumba ya yenye thamani ya Tsh.mil 30 bima yake kwa mwaka haizidi 150,000 .#

" Bima zetu zinaendana na uwiano na kutokana na gharama na thamani, mfano gari uliyonunua kwa gharama ya Tsh.milioni 400 unakatiwa bima ya mil.13 "

"Ni gharama kidogo na nafuu sana ,nikikupa hapa dada yangu 150,000 ambayo ni bima ya nyumba ukienda salun unaweza kusema 150,000 haitoshi ,maana wengine mnanunua wigi la milioni moja ,sasa kwanini usijikatie bima ya nyumba, kilimo ama gari yako  ??!alihoji Kamanga.


Aidha Kamanga alieleza ,bado uelewa kwa wananchi haujawa mkubwa ,kwani wengi wao wanajua bima hizo zinawahusu watu walio matajiri pekee.


Kwa mujibu wake, hakuna elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa bima ya majanga kama ilivyo bima ya afya. Aliwataka wananchi ,kubadilika  na kujiwekea utamaduni wa kujilinda na mali zao kabla ya hatari.

"Tatizo utamaduni tuliojiwekea tunataka kusaidiana likitokea janga la moto, msiba  ,wakati inatakiwa kujiwekea mwenyewe pia kabla ya janga ama shida ,:;"Kizazi kinachokuja inabidi tubadilike na utamaduni huu kama ilivyo kwa wenzetu katika baadhi ya nchi" alisema.

Hata hivyo ,Kamanga alisema ,wamejiwekea kuwa karibu na wananchi kwenye changamoto zao za kijamii ikiwemo afya na elimu. Alisema wameanza kutekeleza katika mikoa ya Iringa, Mwanza, Sumbawanga na wilaya ya Kisarawe -Pwani ikiwa ni miongozo ya utawala bora kwa kushiriki kutatua changamoto ndani ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad