HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 18 May 2018

WAJASIRIAMALI WA ILALA WAOMBA KUKOPESHWA VITENDEA KAZI NA DCB

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa(kulia) katika banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya siku mbili ya wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAJASIRIAMALI  wanawake na Vijana wa Wlaya ya Ilala wameutaka uongozi wa Benki ya DCB kuwapatia mikopo ya vitendea kazi na vifaa kazi ili waweze kujiwekeza vizuri zaidi katika kuendesha viwanda vyao .
Benki ya DCB wamekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa mikopo kwa vikundi mbalimbali vinavyojishugulisha na utengenezaji wa bidhaa za vyakula, nguo, viatu na hata dawa za kusafishia ndani na vyooni. Hayo wameyasema leo wakati wa maonyesho ya siku mbili ya  bidhaa za wajasiramali yaliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa amesema kuwa toka walivyoingia katika makubaliano ya kutoa mikopo na Manispaa ya Wilaya ya Ilala mwaka 2014 kwa wanawake na vijana  tayari wameshaweza kutoa mikopo ya takribani  bilioni 9.2 imetolewa kwa vikundi 2978.
 Ndalahwa amesema kuwa, changamoto iliyokuwepo kwa sasa ni uhitaji wa fedha kwani wanawake na vijana wanaohitaji mikopo hiyo ni wengi katika manispaa na kuiomba Halmashauri kuongeza feda za mfuko huo ili kuwezesha benki kuwahudumia wajasiriamali wengi zaidi.
“Tumelisikia ombi la wajasiriamali la kutaka kuboreshwa kwa mikopo ikiwemo kuongezwa kwa kiasi cha fedha pamoja na kukopesha vitendea kazi na vifaa kazi, sisi kama DCB benki mteja wetu atakapohitaji vifaa atakuja kwetu na tutakaa chini na kuingia makubaliano,”amesema Ndalahwa.
“kuelekea uchumi wa viwanda wanwake na vijana tuzingati ubunifu na kutumia fursa za kiuchumi kupata mitaji na kujiendeleza  na benki itandelea kutoa fursa za mitaji kwa wajasiriamali wa aina hii,”
Akizungumza  baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali hao na kujionea namna wanavyofanya kazi  zao na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli za watanzania kuwekeza zaidi katika shughuli za uzalishaji mali.
Mjema amesema kuwa wajasiriamali hao wameonesha kuwa mikpo waloyokuwa wanaipata imekuwa na msaada mkubwa sana kwao na wameweza kujiendeleza katika kukuza mitaji ya biashara zao na hata wengine waliweza kuanzisha biashara zinine na kujipatia faida.
“Wajasiriamali hawa wameonekana kufikia malengo yaliyowekwa na Rais JPM kwa kuanzisha viwanda, tumeona jinsi gani wameweza kutumia nafasi wakizozipata hususani katika mikopo waliyoipata na kujiendeleza zaidi,”amesema Mjema.
Maonesho hayo yanaendelea kwa  siku  mbili ndani ya viwanja vya mnazi mmoja na dc mjema amewaomba wakina mama na vijana kujitokeza kuja kuona namna wenzao wanavyojishugulisha na ujasiriamali.Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akisalimiana na moja ya waanzilishi wa vikundi vya ujasiriamali Vicky Shayo wakati akitembelea mabanda wakati wa maonyesho ya wajasiriamali yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.


Mjasiriamali Vicky Shayo akizungumza na waandishi wa habari namna walivyoweza kuanzisha kikundi chao na benki ya DCB kuweza kuwapatia mkopo ulioweza kuongeza tija katika miradi yao katika maonyesho ya wajasiriamali yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad