HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 12, 2018

UMOJA WA ULAYA (EU) NA SERIKALI WATANGAZA USHIRIKIANO UFADHILI WA MASOMO YA ELIMU YA JUU ULAYA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiongea na wadau wa Elimu na Utafiti jijini Dar es Salaam Mei 11, 2018, wakati wa kutangaza ushirikiano kwenye masuala ya utafiti na sayansi pamoja na fursa za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kutoka nchi za Umoja wa Ulaya. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Roeland van de Geer alisema Umoja huo una lengo la kufanikisha mpango wa pili wa Maendeleo ya miaka mitano.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer akiongea na wadau wa elimu na utafiti wakati wa kutangaza ushirikiano katika utafiti na sayansi kwa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kutoka Umoja huo.
Wadau wa elimu na utafiti wakifuatilia matukio wakati wa kutangazwa ushirikiano kati ya Serikali na EU katika utafiti na sayansi kwa kufadhili masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo nchi za Umoja wa Ulaya.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer wakiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki hafla hiyo
Picha zote na Robert Okanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad