HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 24, 2018

SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA MAKAZI YA WATU WENYE UKOMA YA SAMARIA HOMBOLO

Serikali imejipanga kuwajengea Kisima cha kisasa watu wenye mahitaji maalum kitachoweza kuhudumia Kaya 26 zenye jumla ya watu 56 wenye ukoma na wazee katika Kambi ya Samaria Hombolo jijini Dodoma.

Hatua hiyo inakuja mara baada ya wakazi wa kambi ya Samaria kueleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo; ukosefu wa maji salama, changamoto za matibabu kwa kukosa bima za afya, uchakavu wa  magodo kwa ajili ya malazi, uhaba wa chakula cha uhakika.

Changamoto hizo zimeibuliwa wakati ya Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa alipoambatana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso Mei 23, 2018 katika Makazi ya watu wenye mahitaji maalum ikiwemo wazee na watu wenye ukoma.

“Watu wenye mahitaji maalum ikiwemo wenye ukoma wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji eneo la Samaria, sisi kama Serikali tumedhamiria kuwajengea kisima cha kisasa kitakachotoa maji baridi na kuweza kuhudumia makambi haya pamoja na kijiji chote cha Samaria”.alisema Naibu Waziri Ikupa

Naye Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameiagiza timu ya waataalamu kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kuanza kazi hiyo mara moja.

“ Naagiza timu ya wataalamu kuja kupima maeneo ambayo yatafaa kwa ajili ya uchimbaji wa kisima hicho” .alisema Aweso

Kwa upande wake, Katibu Chama cha Wenye ulemavu Samaria, Richard Kongawadodo aliipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua ya kujenga kisima cha maji baridi kitakachosaidia kutatua changamoto zilizokuwepo awali na kusaidia katika shughuli za maendeleo ikiwemo za kilimo, umwagiliaji na matumizi mengineyo.

“Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutujali watu wenye mahitaji maalum hasa sisi wenye ukoma kwani tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya kukosa maji ya uhakika na salama, hivyo ujenzi wa kisima hicho utaleta tija hususan katika shughuli za kilimo ili kujipatia fedha na kukidhi mahitaji muhimu”,alisisitiza Kongawadodo

Kwa kumalizia Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Mheshimiwa Mathayo Ndahilo aliwataka wanakijiji wa Samaria kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali pindi inapohitajika ili kufanikisha adhma ya ujenzi wa kisima hicho.

AWALI:

Kituo cha Samari kilianza mwaka 1993 ambacho kipo umbali wa Kilometa Moja na nusu kutoka Hombolo mjini mkoani Dodoma, kwa sasa kinahudumia jumla ya watu wenye ukoma 52 wanaotoka katika Kaya 26 Kijijini hapo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akizungumza jambo na wakazi wa Kambi la wenye Ukoma la Samaria lilipo Kata ya Hombolo Bwawani mkoni Dodoma alipowatemnbelea kutatua changamoto wanazokabiliana nazo tarehe 23 Mei, 2018, kulia kwake ni Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Aweso.
 Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Aweso akiwahakikishia wakazi wa Samaria utatuzi wa changamoto ya maji inayowakabili kwa kuahidi kuanza uchimbaji  wa kisima cha maji baridi baada ya kufanya ziara alipoambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa Mei 23, 2018.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akiwasiliza baadhi ya wakazi wa Kambi la wenye Ukoma la Samaria alipowatembelea Mei 23, 2018 kwa kutatua changamoto ya maji kwa kuahidi kuanza ujenzi wa Kisima cha maji baridi Kijijini hapo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa na Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji (katikati) pamoja na Meneja Kanda ya Kaji kutoka Wakala wa Uchimbaji wa Visima na mabwawa, Khalifu Utali wakiwasililiza wakazi wa Makazi ya wenye ukoma walipowatembelea Mei 23, 2018.
 Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani, Mathayo Ndahilo akitoa maelezo mafupi kuhusu Kituo cha Watu wenye mahitaji maalum cha Samaria wakati wa Ziara ya Manaibu waziri Mhe Stella Ikupa (Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu) na Jumaa Aweso (Wizara ya Maji na Umwagiliaji) walipotembelea Makazi hayo Mei 23, 2018.
 Baadhi ya watu wenye ukoma wanaoishi katika makazi ya Samaria wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa (hayupo pichani) wakati alipowatembelea kutatua baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kambini hapo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso wakikabidhi msaada wa chakula kwa Katibu wa Chama cha Katibu Chama cha Wenye ulemavu Samaria, Richard Kongawadodo kwa ajili ya wanaoishi na ukoma kilichopo Hombolo Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso wakimsikiliza mmoja wa wakazi wa Kambi la Samaria Mzee Simion Lucas walipotembelea kwenye kambi hiyo Mei 23, 2018.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad