HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 24, 2018

PRECISION AIR NA MAXMALIPO WAINGIA MKATABA WA MIAKA MITATU WA HUDUMA KWA WATEJA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Precision Air Sauda Rajab (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal wakitia saini makubaliano ya kimkataba ya huduma za ulipaji 
tiketi kwa njia ya kieletroniki.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirika la ndege la Precision Air limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya MaxMalipo ikiwa ni katika kuboresha huduma za ulipaji wa tiketi kwa njia ya kieletroniki.

Kupitia makubaliano hayo Precision Air itatumia mfumo wa malipo wa MaxMalipo kuwezesha wateja wake kulipia tiketi tiketi zao kwa njia ya malipo ya mitandao ya simu, Benko na Mawakala wa MaxMalipo.

Akizungumza baada ya kuwekeana saini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Sauda Rajab utakuwa na faida kwa wateja wa Precision Air kulipia tiketi zao kwa urahisi zaidi ambapo watalipa kwa njia ya simu kupitia mitandao yote ya simu za mkononi, malipo kupitia akauntibza benki zinazokubali malipo kupitia mfumo wa MaxMalipo na mawakala wote nchini takribani elfu thelathini (30,000).

Sauda amesema kuwa, makubaliano haya ni kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Juni 2017 hadi Juni 2020 na kukiwa na mkakati wa ongezeko la abiria kwa asilimia 20 hadi 30 kwa mwaka wa kwanza mkataba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision Air Sauda Rajab akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia nakubaliano na kampuni ya MaxMalipo, kulia ni Makurugenzi Mkazi MaxMalipo Tanzania Charles Natal.

"Mkataba wetu na MaxMalipo ambapo ni wa miaka mitatu umewekewa makubaliano ya ongezeko la abiria ambapo kwa mwaka tunachukua takribani wateja laki nne (400,000) ila mkakati uliowekwa zaidi ni kufikia malengo ya kuongeza wateja kwa asilimia 20 hadi 30 kwa mwaka wa kwanza,"amesema Sauda.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo nchini Tanzania Charles Natal  amesema kuwa ubia huu baina ya MaxMalipo na Precision Air unawezesha wateja wote kufanya malipo ya tiketi za usafiri wa ndege kwa urahisi zaidi na kwa haraka.

Amesema kwa sasa MaxMalipo ipo katika nchi tano za Afrika na ikiwemo Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia na tayari nchini Kenya wataanza huduma zao hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uwekaji saini makubaliano na Shirika la Ndege la Precisio  Air kwa ajilo 
ya huduma za ulipaji wa tiketi kwa njia ya Kieletroniki, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air Sauda Rajab na Meneja Masoko na Mawasiliano Precision Air Hillary Mremi

"Tumejizatiti zaidi kutoa huduma za malipo ya tiketi kwa njia ya kieletroniki badala ya kufanya booking online au kupitia kwenye ofisi za Precision Air na kupatiwa nambari ya malipo (booking reference number),"amesema Natal.

Mkataba huo umesainiwa mbele ya waandishi na wahabari na kubadilishana hati za makubaliano hayo kuonyesha kuanza kazi mara moja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision Air Sauda Rajab na Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal wakipeaa mikono baada 
ya kubalishana hati za makubaliano baina yao. 

Picha ya pamoja baina ya uongozi wa Precision Air na MaxMalipo Tanzania.Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air Sauda Rajab, Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal. Meneja Masoko Na Mawasiliano Precision Air Hillary Mremi na Mkuu wa Kitengo cha Biashara Deogratius Lazaro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad