HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 8 May 2018

Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini

Wapenzi wa Soka vijiji kufurahia michuano ya Kombe la dunia mwaka huu. Hii ni kutokana na Kampuni ya Star Times ambayo ina mkataba hapa nchini wa kutangaza mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2018, yatakayofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi ujao, Kampuni hiyo imeingia ushirikiano na kampuni ya kusambaza nishati ya  jua na vifaa vinavyotumia nishati hiyo ya Mobisol, kutumia mtandao wake kuwezesha wananchi wanaoishi maeneo yasio na  umeme wanaotumia nishati ya umeme wa jua nchini na nchi jirani za Kenya na Uganda kutokupitwa na mashindano hayo ya kihistoria duniani kote.

Ushirikiano huo ambao umetangazwa jijini Dar es Salaam leo unawezesha wateja wanaotumia umeme na vifaa vya  Mobisol  kununua vifaa  maalumu  vya kuboresha mawasiliano vitakavyowezesha kushuhudia mechi za kombe la dunia, sambamba na kupata chaneli mbalimbali za burudani kupitia vingamuzi vya Star Times.

Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mobisol Tanzania,Patric Juma,ameeleza kuwa wateja wa Mobisol nchini, wanaweza kununua vifaa vya mawasiliano kutoka star Times vitakavyowawezesha kufurahia burudani hiyo ya soka  bure na kwa wakati wote kuanzia sasa hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu.Vifaa hivyo baada ya kununuliwa wanafungiwa bure  popote walipo.

“Tunafurahia kuingia ushirikiano huu na Star Time,hasa kwa kuwaletea ofa maalumu wananchi wanaotumia umeme wa nishati ya jua maeneo mengi yasiyo na umeme ili kuwawezesha kupata burudani za mashindano ya Kombe la Dunia ,Mobisol tutahakikisha tunaendelea kusambaza umeme kwenye maeneo yasio na nishati hiyo sambamba na kubuni vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati ya jua”Alisema Patric Juma.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Star Times nchini Tanzania, Walker Wang ,alisema “kampuni yao inayo furaha kufanya kazi na Mobisol katika kuhakikisha familia nyingi zinazotumia umeme wa mtandao wake wanaweza kutumia ving’amuzi vyao  na vifurushi maalum vitakavyowawezesha kuangalia mashindano ya Kombe la Dunia ambapo kampuni yao ndiyo yenye hakimiliki ya kutangaza mashindano haya makubwa ya soka duniani.”

Kampuni ya Mobisol imeweza kusambaza umeme wa  jua wenye nguvu mpaka 10MW kwa kaya zaidi ya 500,000 katika nchi za Afrika Mashariki pia inasambaza vifaa bora na vya kisasa vinavyotumia umeme wa jua kwa gharama nafuu vyenye uwezo wa kutumia umeme wa 40W hadi 200W,vifaa ambavyo inasambaza mbali  na vya kuwasha na kuchaji  simu pia inasambaza  vyombo vya muziki na Televisheni bapa za kisasa  zenye ukubwa tofauti.
 Makamo wa Rais wa Startimes,Zuhura Hanif(kulia)akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu (wapili kushoto)baada ya Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Wengine kushoto ni Meneja wa Mobisol Lynda Okoko pamoja na Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa.Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa kampuni ya Umeme wa Jua-Mobisol,Lynda Okoko(kushoto)akipeana mkono na Makamo wa Rais wa Startimes kuashiria Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi,Wengine katika picha wapili kushoto ni Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa na Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa kampuni ya Umeme wa Jua-Mobisol,Lynda Okoko, Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa,Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu pamoja na Makamo wa Rais wa Startimes Zuhura Hanif,wakionyesha vipeperushi vyenye chaneli mbalimbali zitakazorusha kombe la Dunia  wakati wa Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu(kushoto)akiwaonesha vifaa vya umeme wa Jua,Makamu wa Rais wa Startimes Zuhura Hanif na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa,vitakavyotumika kurusha soka msimu wa Kombe la Dunia 2018  wakati wa Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo hiyo msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad