HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 3 May 2018

Mkongwe Ndimara ataka serikali kutopewa sababu ya ‘kubana’ waandishi wa habari

Na Mwandishi wetu, Dodoma
WAANDISHI wa habari wanapaswa kuandika na kutangaza habari zao kwa weledi na kuzingatia maadili ili kuepuka kuandika habari zinazoipa serikali sababu ya kufungia vyombo vyao.
Kauli hiyo imetolewa mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania Bw. Ndimara Tegambwage wakati akitoa mada ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania kwenye kongamano la maadhimisho ya siku ya Uhuru Wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo nchini Tanzania yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Kila Mei 2-3 kila mwaka ni siku za kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani.
Aidha katika mada yake hiyo Ndimara alisema Serikali barani Afrika zimekuwa zikikosa uvumilivu na kunyima uhuru vyombo vya habari licha ya kuwa uhuru huo unatambuliwa na katiba za mataifa ya Afrika.
Bw. Ndimara amebainisha kuwa, wakati serikali za Africa zikitoa haki ya kusajili vyombo vya habari hususani Radio, Runinga na Magazeti, serikali zinapokosolewa huvifungia vyombo hivyo kwa tuhuma za kukiuka maadili jambo ambalo alidai kuwa si la ukweli.
Mkongwe huyo wa tasnia ya habari nchini Tanzania amebainisha kuwa serikali nyingi barani Afrika zimekosa uvumilivu na kutumia nguvu nyingi kunyamanzisha wanahabari.
Huku akinukuu hotuba ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ambaye ameonya kuwepo kwa wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya aliwataka waandishi wa habari kuwa makini kutokana na sheria mbalimbali zinazowazunguka zinaohitaji weledi wa hali ya juu katika kuhabarisha.
Awali akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania, Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema Tanzania inautambua mchango wa vyombo vya habari katika kurahisisha mawasiliano ya jamii na kuharakisha maendeleo lakini inakwazwa na kuwepo kwa baadhi ya vyombo vya habari na wanahabari ambao huandika habari nyingi za kutungwa na za uongo.
Katika hotuba hiyo alilaani matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii akitaja kuwa inaongoza kwa kuwa na habari nyingi za kujitungia na zenye upotoshaji na kwamba Bunge ni mhanga wa upotoshaji wa habari zinazoandikwa na baadhi ya waandishi katika mitandao ya kijamii.
Akizungumzia ufanisi wa vyombo vya habari na wanahabari wenyewe Spika Ndugai aliwataka waandishi kuwa marafiki na kuacha tabia za kudharauliana  na kushauri ipo haja ya kuwekana sawa kwa maslahi mapana zaidi ya kitaaluma na jamii kwa ujumla.
Pia alizungumzia vyombo vya habari kusaidia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi na kusema kalamu ikitumika vyema itasaidia sana mapambano hayo.
“Wajibu mwingine wa vyombo vya habari ni mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, lakini zoezi  hili huwa na matokeo chanya kama litazingatia ukweli na maadili yaliyopo” alisema Spika Job Ndugai na kuongeza kuwa bunge linajua changamoto zilizopo na kwamba wapo tayari kutoa ushirikiano.
“Bunge letu linajua changamoto ambazo baadhi ya wanahabari mnazipitia, tuko tayari kushirikiana nanyi kuona tasnia yetu ya habari inaboreshwa”  alisema Ndugai.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit amesema vyombo vya habari ni muhimu kwa maendeleo kwa hiyo ni lazima viwe huru ili viweze kutekeleza kazi yake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, alieleza kusikitishwa kwake na matukio yanayoashiria kubinya uhuru wa vyombo vya habari  na pia kuitaka serikali kuwajibika katika kuwalinda waandishi wa habari.
Wawakilishi wa radio jamii Tanzania wanasema pamoja na kufanyakazi kubwa ya kuelimisha jamii vijijini, serikali haijavipatia kipaumbele kama inavyofanya kwa vyombo vikubwa na vya kitaifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Kiongozi wa Kituo cha Habari cha mkoani Radio FM cha visiwani Pemba Bw. Maalim Ali Abass alisema Radio za vijijini zinapokumbwa na kosa lolote la kitaaluma mema mengi wanayofanya kwa kujitolea husahaulika haraka na kujikuta katika hekaheka na serikali.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung Tanzania, Andreas Quasten (kushoto) pamoja na Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem (kulia) wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndenjembi akisalimiana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari zinazofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Kushoto ni Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem
 Mshehereshaji wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Innocent Mungy (katikati), Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu wa Ubalozi wa Sweden nchini, Anette Widholm Bolme (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Gasirigwa Sengiyumva wakipitia ratiba ya maadhimisho hayo yanayofanyika katika hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akisalimiana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndenjembi (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa tatu kushoto), Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem (wa pili kulia) pamoja na Mshehereshaji wa kongamano hilo, Innocent Mungy (kulia).
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai (wa tatu kulia) akiongozana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (kulia), Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndenjembi (kushoto) kuelekea kwenye mabanda ya maonyesho mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipitia nakala ya gazeti la Majira huku akipata maelezo kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira, Imma Mbuguni (wa pili kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Kulia ni Meneja Usambaza wa Gazeti la Majira, Sophia Mshangama.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mjenga Uwezo wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Deogratius Bwire kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao huo  mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari zinazofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Deo Ndenjembi (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa tatu kushoto)
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipokea nakala ya gazeti la Mwananchi kutoka kwa wafanyakazi wa Mwananchi Communications wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipata maelezo kutoka kwa Mmoja wa Wakurugenzi na Mmiliki wa Gazeti la Jamhuri Deodatus Balile wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipokea majarida na machapisho mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kutoka Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo wakati alipotembelea banda la UN kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai kuhusiana na kitabu cha Maadili ya Uandishi wa Habari wakati alipokuwa akitembelea banda la Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Logistic wa Baraza hilo, Athuman Mbegu.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano tayari kuanza kwa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mshehereshaji wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Innocent Mungy akiwakaribishwa meza kuu, wanahabari na wadau wa habari kwenye kongamano la  maadhimisho hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Meza kuu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akifungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akitoa salamu za Unesco wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai kufungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumzia malengo ya maendeleo endelevu na jukumu la waandishi wa habari kutumia nafasi zao kutoa taarifa kuhusu malengo hayo kwa jamii ili yatekelezeke kwa urahisi, katika kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa kujitegemea, Rose Haji Mwalimu akiongoza mjadala kuhusu mada: Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana inatendeka wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mwandishi wa Habari Nguli, Ndimara Tegambwage na mwezeshaji wa mada inayohusu; Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana inatendeka: wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Wakili na Mwandishi wa Habari ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, James Marenga akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Nashera jijini Dodoma.
 Mdau wa Habari Ernest Sungura akishiriki kuchangia maoni katika mjadala uliowasilishwa na mwandishi nguli Ndimara Tegambwage (hayupo pichani) wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege (kulia) na Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu wa Ubalozi wa Sweden nchini, Anette Widholm Bolme wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Pichani juu na chini Sehemu ya washiriki ambao ni wahariri, waandishi wa habari, wadau wa tasnia ya habari na wageni waalikwa waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wakiwemo wahariri, wadau wa habari na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa habari na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, Ubalozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari vya kijamii waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja waandishi wa habari wakonge (Veterans) waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja mameneja wa redio za kijamii waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja wanafunzi wa Dodoma College of Journalism waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad