HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 6, 2018

MAKAMU MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AWAONGOZA WANANCHI KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE YA MSINGI NYANDOTE WILAYANI RUFIJI

NA ELISA SHUNDA, MUHORO-RUFIJI

WANANCHI na Wadau mbalimbali waombwa kushikamana kwa pamoja na kuondoa tofauti ya itikadi za kivyama na kushiriki kwa pamoja kuisaidia serikali katika ukuzaji wa maendeleo ya jamii katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Mazingira na sekta ya Miundombinu.



Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mh. Haji Haidari kwenye harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote iliyopo Kata ya Muhoro wilayani Rufiji ambapo alisema kuwa hadi jumuiya hiyo ya wazazi kufikia uamuzi wa kufanya harambee ya ujenzi wa shule hiyo ni kutokana na umbali uliopo wa Kilometa 12 kutoka kwenye Kijiji cha Nyandote na Shule ya Msingi Muhoro hali iliyosababisha wanafunzi walio wengi kutomaliza shule kulingana na changamoto mbalimbali ikiwemo kubakwa na kulawitiwa njiani na watu waovu,mimba,njaa na umbali wa shule ilipo.



“Nawapongeza wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama na jumuiya zake kwa kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha tunafanikisha harambee hii ya ujenzi wa shule ya msingi ya Nyandote ambapo si kwa faida ya watoto wa wanachama wa CCM peke yake bali ni watoto wa jamii nzima nawashukuru sana kwa mlivyojitoa.



“Kwa kujitolea kwenu huku shule ya msingi Nyandote ikikamilika tutakuwa tumewasaidia wanafunzi 430 kuanza masomo yao lakini pia tutakuwa tumewaepusha wanafunzi hao na kutembea umbali mrefu wa Kilometa 12 kuja shuleni Muhoro pia tutawaepusha na vishawishi mbalimbali za njiani,tutawaokoa na kubakwa na kulawitiwa njiani na watu waovu” Alisema Mh.Haidari



Aidha akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Pwani Jackson Kituka aliwapongeza wenyeviti wake wa jumuiya hiyo wa wilaya kwa umoja wao kuamua kushirikiana katika kuleta maendeleo katika jamii zinazowazunguka kwa kutafuta wadau mbalimbali wa kusaidia sekta zinazohusiana na jumuiya hiyo na kuzisihi jumuiya zingine kuiga mfano kwa jumuiya hiyo kongwe kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).



“Nawapongeza sana wenyeviti wote wa jumuiya za wazazi wilaya zilizopo katika Mkoa huu wa Pwani kwa ushirikiano mnaonyesha endeleeni hivyo hivyo msitengane,nampongeza Mwenyekiti wa Uchumi Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Rufiji,Juma Salum Mpendu “Chogo” kwa kuamua kujitolea kuchangia Simenti mifuko 100,Lori nne za mchanga kwa ajili ya ujenzi wa shule hii ya Nyandote na amechangia Sh.200,000 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya choo shule ya msingi Muhuro lakini pia bila kuwasahau wananchi wote wa Kata ya Muhoro waliochangia Sh.220,000” Alisema Mwenyekiti Kituka.



Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Kibaha mjini,Edwin Shunda alisema kuwa baada ya kupata taarifa ya harambee hiyo alihangaika kuzungumza na wadau mbalimbali kuhusu jambo hilo kwa bahati nzuri amefanikiwa kupata mifuko 100 ya Simenti iliyotolewa na aliyekuwa MNEC wa Kibaha Mh.Rugemalira Rutatina kama mchango wa jumuiya hiyo ya wazazi Kibaha mjini kwa ujenzi wa shule hiyo ya msingi ya Nyandote.



Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mkuranga,Khamis Mtutu ameahidi kutoa mifuko 30 ya Simenti kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo kama njia mojawapo ya kumuunga mkono mwenyekiti mwenzao Abdul Mayoyola wa wilaya ya Rufiji.



Hata hivyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Rufiji,Abdul Mayoyola ametoa shukrani kwa wenyeviti wenzake wa jumuiya hizo wa wilaya walioweza kushiriki katika harambee hiyo na kuchangia kile walichojaliwa na kuwaomba wazidi kushikamana kwa jambo lolote litakapotokea sehemu nyingine kwa maendeleo ya Mkoa wa Pwani.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa eneo hilo kwenye mkutano huo wameishukuru Jumuiya ya Wazazi ya CCM kwa upendo wao kuamua kuchangisha fedha na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ya Nyandote ambapo itasaidia watoto wao kupata elimu na kuondokana na kadhia ya njiani na umbali mrefu.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji (katikati) akikabidhi mifuko 230 pamoja na fedha taslimu Sh. 650,000 kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote iliyopo Kata ya Muhoro Wilayani humo jana. Picha zote na Elisa Shunda. 
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Muhuro,Mary Msigwa (katikati) akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji (kulia) kuhusu kupokea mifuko 230 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote na amekabidhiwa Sh. 440000 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya choo kwenye shule ya Msingi ya Muhuro iliyopo wilayani Rufiji.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji akizungumza na wananchi kuhusu kupokea Sh.200,000 na Mifuko ya Simenti 100 kutoka kwa Mwenyekiti wa Uchumi Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Rufiji,Juma Salum Mpendu “Chogo” kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la Nyandote
Wazee wakifuatilia kwa umakini mkubwa mkutano huo wa harambee.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Pwani, Jackson Kituka akizungumza kwenye mkutano huo wa harambee.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Charles Makunga akizungumza kwenye mkutano huo wa harambee.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Pwani,Gama J. Gama akifafanua jambo kwenye mkutano huo.

Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mh.Harusi Nkenda akizungumza na wananchi wa Kata ya Muhoro kuhusu kujitolea kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla pasipo kuangalia itikadi ya kivyama,lakini pia amewakumbusha wananchi hao kuwa wasafi majumbani mwao ili wajiepushe na magonjwa ya mlipuko kama ugonjwa wa Kipindupindu,Pia hakusahau kuwapa pole kwa wananchi wote waliokumbwa na kuwapoteza ndugu zao katika kipindi kifupi kilichopita ambacho viongozi wa Chama Cha Mapinduzi walikuwa wakishambuliwa na kuuawa na watu wasiojulikana.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wa Wilaya ya Rufiji,Abdul Mayoyola.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Mkuranga,Khamis Mtutu akizungumza kuhusu kuchangia mifuko 30 ya simenti kwa ajili ya kujenga shule ya msingi ya Nyandote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad