HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 24 May 2018

Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mtayarishaji na muigizaji wa filamu hapa nchini  Laurent Matiholo maarufu kama “Makala” amefunguka na kuweka wazi juu ya  ukaribu wake wa kimahusiano na msanii mwenzake Jeniffer Kyaka maarufu kama ”Odama”.

Makala ambaye  alijipatia umaarufu mkubwa sana tasnia hii ya filamu,baada ya kupokelewa vema na mashabiki katika kazi zake zilizomtambulisha vema kwenye ulimwengu huo zikiwemo  filamu ya Kiss Me, Hot Love, Shella, Surprise na nyingine kibao alizocheza katika kiwango cha hali ya juu na kujipatia umaarufu mkubwa na ndani na nje ya nchi akiwa chini ya Mtunzi na Mtayarishaji nguli  Mussa Banzi.

 Makala amesema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii, zikimuhusisha kuwa na ukaribu ambayo ukifananishwa na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake kitu ambacho akina ukweli wowote.

“Unajua Bongo kumekuwa na mambo mengi sana na watu hata hawajui tumetoka wapi na Odama wanaanza kusambaza uzushi wa mimi kutoka kimahusiano nae, taarifa hizo wanazosambaza hawana uhakika nazo na laiti Wangejua navyomchukulia huyo dada kama nimezaliwa naye tumbo mmoja wala waingethubutu kunipakazia najisikia vibaya,"amesema Makala.

Amesema kuwa katika  mafanikio yake Odama amekuwa na mchango mkubwa sana kama dada yake na  amempiga tafu sana na anatamani siku moja aje kufikia alipokuwa yeye kwa sasa.

Makala ni  mmiliki wa kampuni ya Usambazaji inayofahamika kama Wa Ukweli na  kwa sasa anatamba na filamu ya Big SURPRISE  inayokimbiza kwenye tasnia ya filamu akicheza na  wakali wenzake wakiwemo Gabo,Odama,Mzee Jengua na wengine kibao,yupo njiani kuachia kazi mpya nyingine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad