HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 31, 2018

KITENGO CHA LISHE KUTOA MATONE YA VITAMIN A NA DAWA ZA MINYOO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA SITA

 Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Wizara ya Afya Zanzibar itaanzisha zoezi la mwezi mmoja la utoaji matone ya Vitamin A na Dawa za Minyoo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kuanzia Juni 1, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa jengo la Malaria Mwanakwerekwe, Msimamizi wa Lishe Wilaya za Magharibi Salama Makame amesema zoezi hilo litafanyika katika vituo vyote vya afya kwa siku za kazi na siku za Jumamosi na Jumapili zoeli hilo litaendelea ndani ya shehia katika vituo maalum vitakavyopangwa.

Aliwataka wazazi na walezi ambao hawatapata nafasi ya kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya kwa siku za kazi kuwapeleka katika vituo vitakavyopangwa kwenye shehia zao ili kupata matone ya Vitamin A na Dawa ya Minyoo.

Alisema lengo la Wizara ya afya kutoa matone ya ya Vitamin A na Dawa ya Minyoo kwa watoto wenye umri kuanzia miezi sita mpaka miaka mitano ni kuwaepusha na maradhi mbali mbali na kuwawezesha kukua vizuri wakiwa na afya bora.

Bi. Salama aliongeza kuwa tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa tokea kuanzishwa zoezi la kutoa matone ya Vitamin A na Dawa ya Minyoo kwa watoto imesaidia kupunguza  idadi ya vifo vya watoto hao kwa asilimia 33.

Alisema Wizara ya afya imejiandaa kuwafikia zaidi ya watoto laki mbili elfu sita Unguja na Pemba, hivyo amewashauri wazazi kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao ili kufikia malengo ya yaliyowekwa.

Alikumbusha kwamba katika zoezi lililofanyika mwezi Novemba mwaka jana, watoto waliopatiwa Matone ya Vitamn A na Dawa ya Minyoo ilifikia asilimia 98 na ametaka zoezi la mwaka huu lizidi matokeo ya mwaka jana.
 AFISA Msimamizi wa Chanjo Wilaya ya Magharibi ‘A’ na ‘B’ Salama Makame Ashrak akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana zoezi la utoaji wa Matone ya Vitamen A  na dawa za Minyoo linaloanza tarehe 1 June 2018 na kumalizika tarehe 30 Juni 2018. katika ukumbi wa Malaria uliopo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
MWANDISHI wa habari wa Star TV Abdalla Pandu akiuliza Maswali  kuhusu zoezi la   utolewaji Matone ya Vitamen A na dawa za Minyoo katika ukumbi wa Malaria uliopo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar( Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad