HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 25, 2018

IDARA YA UHAMIAJI YAZINDUA PASIPOTI YA KIELEKTRONIKI DAR ES SALAAM, WAKAZI WAHIMIZWA KUZICHANGAMKIA


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jami
PASIPOTI ya kieletroniki imezinduliwa leo na Idara ya uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa na Rais mapema Januari mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi huo kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameeleza pasipoti hiyo ina manufaa makubwa hasa katika teknolojia, kukidhi viwango vya kimataifa na kufafanua ukiwa nayo unakuwa na nakala ya pasipoti kwenye simu mara baada ya kupakuwa applicationi hiyo.

Mhandisi Ndikilo ameeleza gharama za kupata pasipoti hiyo ni Sh.150,000 na kueleza kuwa pasipoti za kawaida zitaendelea kutumika hadi Januari 2020.

Aidha ametoa rai kwa wananchi hasa katika utunzaji wa pasipoti hizo ili zisiangukie kwa wahalifu na gharama kwa pasipoti iliyopotea mara ya kwanza ni shilingi laki 5 na ikipotea kwa mara ya pili italipiwa shilingi laki 7 na nusu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewaomba wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam wachangamkie fursa hiyo, pia ametoa wito wa kada mbalimbali hasa wafanyabiashara wadogo kupata pasipoti hizo ili kuweza kufanya biashara kwa uhuru na kuvuka mipaka hii itawasaidia kutangaza biashara zao.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Chrispin Ngonyani amehaidi kusimamia kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa na amewaomba wananchi kueleza changamoto wanazokumbana nazo ili ziweze kutatuliwa mara moja.

Pia, Kamishina wa Uhamiaji, uraia na pasipoti Gerald Kahiga ameeleza kuwa pasipoti hizo zinatolewa kwa raia wa Tanzania pekee na zikitolewa wazitunze kwa usalama wa hali ya juu na wamejipanga na harufu yoyote ya rushwa katika utoaji wa pasipoti hizo na ametoa rai kwa wananchi kutotumia mawakala kama daraja la kupata pasipoti hizo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Cathy Kamba amefurahishwa na uzinduzi huo kwani hata katika ilani ya uchaguzi walisisitiza suala la ulinzi na usalama na amemshukuru Rais kwa kuendelea kuboresha maisha ya watanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad