HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 31 May 2018

BREAKING NEWS: ZINEDINE ZIDANE AACHIA NGAZI REAL MADRID

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Real Madrid, Zinedine Zidane 'Zizzou' mchana wa leo ametangaza kuachia ngazi kama Kocha Mkuu wa kikosi hivyo baada yakutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE).

Zidane (45) alijiunga na Real Madrid mwaka 2014 akianza kukinoa kikosi cha Castilla (Real Madrid B).

Zidane alichukua mikoba ya Rafael Benitez aliyeondoka kwenye Kikosi cha kwanza hapo January 2016 .

Kwenye Mkutano wake na Waandishi wa Habari nchini Hispania, Zidane ameeleza kwamba: "Kila kitu kina mabadiliko na ndio maana nimefanya maamuzi haya, naipenda Madrid".

"Nafikiri Madrid inahitaji kushinda mataji zaidi, nafikiri pia mabadiliko yanahitajika", ameongeza Zizzou. 

Alipata mafanikio na Real Madrid kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuiondoa Atletico Madrid kwenye Fainali ya Michuano hiyo barani Ulaya, alipatetea Kombe hilo mwaka unaofuata na kuweka historia mpaka sasa licha yakukosa taji la La Liga msimu wa 2017-2018

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad