HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 25 May 2018

BENKI YA CRDB YANG'ARA TUZO YA BENKI BORA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI

 Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

TUZO kwa benki bora Afrika mwaka 2018 zimetolewa jijini Busan Korea Kusini huku aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Profesa Benno Ndulu na Benki ya CRDB wakitwaa tuzo.

Hivyo tuzo hizo zimetolewa katika mkutano wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) na kusherekea maendeleo na huduma za benki barani Afrika.


Katika tuzo hizo aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Profesa Benno  Ndulu ametwaa tuzo ya Gavana Bora Afrika 2018 na hiyo ni kutokana na mchango wake katika kukuza huduma za kifedha kwa wananchi.

Aidha Benki ya CRDB imeshinda Tuzo ya Benki bora katika Ukanda wa Afrika  Mashariki huku katika ukanda wa Magharibi benki ya BDM kutoka mali ilichukua tuzo, ukanda wa kaskazini benki ya CCB ya Misri ilichukua tuzo, ukanda wa Afrika ya kati benki ya BGFI ya Gabon ilitwaa tuzo na ukanda wa kusini benki ya State Bank Mauritus (SBM) ilitwaa tuzo hizo.

Pia tuzo hizo zimetolewa kwa benki bora Afrika ambapo tuzo imeenda kwa benki ya Equity ya nchini Kenya chini ya uongozi wa James Mwangi na hiyo ni kutokana na benki hiyo kukua katika mifumo ya ugunduzi na uwekezaji bila kutegemea mikopo kutoka kwa wateja.


Pia tuzo zilizotolewa ni pamoja na zile zilizofanya vyema katika sekta za uwekezaji na masuala ya uwekezaji ambapo  Afrika Kusini, Malawi na Msumbiji waliibuka kidedea.

Omar Ben Yedder   mmoja wa waandaaji wa tuzo hizo ameeleza kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa tuzo hizo kutolewa nchini Korea na hiyo ni kutokana na nia ya dhati ya Korea Kusini kudumisha mahusiano na nchi za Afrika.

Pia ameeleza washindi wa tuzo hizo wameakisi hali halisi hasa katika masuala ya miundombinu na uwekezaji katika nchi za Afrika na kuzitaka kujikita zaidi katika masuala ya uwekezaji na utoaji wa huduma bora kwa wateja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad