HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 3 May 2018

BASF yafungua ofisi mpya Tanzania

 BASF, ambayo ni kampuni ya kemikali inayoongoza duniani, imezindua ofisi zake mpya jijini Dar es salaam, Tanzania.

Ofisi hiyo ilizindliwa na Balozi wa Balozi wa Ujerumani Tanzania Detlef WaechterJijini Dar es Salaam huku akiipongeza BASF kwa hatua hiyo kubwa.

Makamu wa Rais wa BASF Afrika, Bw. Michael Gotsche alisema, “Ujio wetu nchini Tanzania utatuwezesha kuchangia katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na hali ya ushindani sokoni na wakati huo huo kutuwezesha kuwafikia.”

Alisema ofisi hiyo itatoa huduma za mauzo pamoja na msaada wa kiufundi kwa wateja wa BASF Tanzania.

Alisema BASF ilianza kufanya biashara katika bara la Afrika kama miaka 90 iliyopita ikielekeza nguvu zake kwenye sekta za viwanda zikiwemo ujenzi, nguo, magari, kilimo, plastiki na sekta ya afya.

Alisema Uzinduzi wa ofisi mpya Tanzania utapanua wigo wa BASF barani Afrika na utaongeza ushirikiano kati ya BASF na makampuni ya Kitanzania uliojaa ubinufu mkubwa na utakaolenga ukuaji endelevu.

Alisema miongoni mwa mikakati ya ukuaji wa kampuni ya BASF barani Afrika ni kuwekeza kwa kuwa na uwepo wa ndani na uzalishaji wa ndani wa nchi husika. BASF katika miaka ya hivi karibuni imefungua ofisi zake nchini Zambia, Ivory Coast and Kenya.

“Siku zote hapa BASF huwa tunafanya tathmini ya utendaji wa kiuchumi wa kampuni na kuchukua hatua stahiki zitakazo tuelekeza katika hatua husika zitakazotuwezesha kutanuwa wigo kuingia kwenye masoko mapya na kurahisisha upatakinaji wa bidhaa zetu kwa wateja wetu,” alisema Gotsche.

Kutokana na uzoefu wa kitaalamu na upana wa huduma na bidhaa wanazotoa kuanzia bidhaa za utendaji, plastiki, kemikali, mafuta na gesi pamoja na bidhaa za ulinzi wa mazao, BASF inalenga kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma na msaada wanaohitaji.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa BASF Tanzania, Bw. Mats Idvall, kipaumbele cha BASF ni kuvuka matarajio ya wateja wake. “Tanzania inawakilisha kitovu cha uchumi wa viwanda kwa biashara nyingi kutokana na mazingira yake mazuri ya kiuchumi yalio imara”, alisema. “Kuanzishwa kwa ofisi hizi mpya unadhihirisha ni kiasi gani BASF imejitolea kukuza biashara katika soko hili muhimu sana kimkakati”, aliongeza.
Balozi wa Ujerumani Tanzania Detlef Waechter akikata utepe kuzindua rasmi ofisi za BASF Tanzania katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa BASF Tanzania Mats Idvall, Makamu wa Rais BASF Afrika, Michael Gotsche na Malin Idvall ambaye ni mke wa Mkurugenzi wa BASF Tanzania.

Balozi wa Ujerumani Tanzania Detlef Waechter (kulia) akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa ofisi za BASF Tanzania Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kusoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BASF Tanzania Mats Idvall na  Makamu wa Rais BASF Afrika, Michael Gotsche.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad