HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 25 May 2018

BALOZI WA POLAND NCHINI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski akilakiwa na wenyeji wake alipo wasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam yaliyopo wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Balozi huyo ametembelea Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.
Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (kulia) akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi. (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye aliyeketi (mbele) akisoma taarifa ya Jeshi hilo kwa Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kulia) alipotembela Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (kushoto), akimsikiliza kwa makini msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia) wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi. (Wa pili kulia) ni Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kushoto), wengine ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (wa pili kulia), Kamishna wa Usalama Dhidi ya Moto, (CF) Jesuald Ikonko (wa kwanza kushoto) na msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia).
Picha ya pamoja.
(Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad