HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 5 April 2018

TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekutana  na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa kwa ajili ya kupata miongozo ya kufanya kiwanda kiweze kujengwa  na kuanza kuzalisha dawa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Adam Fimbo amesema kuwa kuwakutanisha wadau hao umetokana mkutano wa Mawaziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto ambapo TFDA imeona ni muda mwafaka katika kuweza kuwapa muongozo wadau jinsi ya kuweza kuanzisha viwanda hivyo.

Fimbo amesema kuwa TFDA kazi yake kubwa ni kuangalia usalama wa dawa tangu inapozalishwa mpaka inaingia sokoni ikiwa lengo ni kumlinda mlaji na dawa hizo.

Aidha amesema kuwa ili kiwanda cha dawa kiweze kusajiliwa na kuzalisha dawa hizo lazima vigezo vilivyowekwa vizingatiwe.

Fimbo amesema baada ya kupata michoro wa ramani pamoja na ujezi na kuanza kuzalisha dawa usajili hauzidi siku 15 kutokana na hatua zote zilizofanyika TFDA inakuwa imepitia.

Hata hivyo amesema kuwa hakuna urasimu wowote katika kusajili dawa au kiwanda nia kumlinda mlaji kwa dawa anazotumia.

“Bila kuwa na usalama wa dawa unaweza ukaua watu ndio maana TFDA tuka kwa ajili ya kazi hiyo ya kuangalia usalama wa dawa za ndani na zinazoingia”amesema Fimbo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Adam Fimbo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kukutana  na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa kupata miongozo  ya kufanya kuwekeza katika sekta hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mkaguzi wa Viwanda vya Dawa wa TFDA, Proche Patrick akiwapitisha katika miongozo wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa  leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Msajili wa Dawa wa TFDA, Dk. Shani Maboko akizungumza  na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa jinsi ya usajili wa dawa unavyofanyika katika mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa wakisikiliza mada zinazotolewa na TFDA leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad