HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 10, 2018

TECNO CAMON X NA X PRO ZATAMBULISHWA RASMI

Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING ambayo ni kampuni mama ya TECNO, Andy VAN (Wapili kutoka kushoto) wakionesha simu aina ya Tecno  CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3 mara baada ya kuzindua simu hiyo.
 Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING ambayo ni kampuni mama ya TECNO, Andy VAN  (Katikati)akizungumza na wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Tecno ambayo ni Tecno CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3.
KAMPUNI ya simu za mkononi inayofanya vizuri barani Afrika inaendelea kutanua soko lake baada ya kuzindua simu mpya TECNO CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3, ikiwa ni muendelezo wa toleo la ‘TECNO CAMON’ iliyozinduliwa nchini NIGERIA (LAGOSI), Tarehe 5/4/2018.

Katika uzinduzi huo TECNO imejihakikishia uzalishaji na usambazaji wa simu zenye technolojia na ubora zaidi katika masoko zaidi ya 40 hasa katika nchi za Afrika. Kampuni ya simu ya TECNO hivi karibuni imeweza kuingia mkataba na moja kati ya kampuni bora katika upande wa mitandao (GOOGLE) iliyozindua mfumo mpya ya uendeshaji wa simu za mkononi Android 8.0Oreo (Go edition), utakaotumika katika matoleo yote ya TECNO kwa ndani ya mwaka 2018.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING Sambayo ni kampuni mama ya TECNO, Bwana Andy VAN amesema, “TECNO haizalishi simu kwa kuzingatia maoni ya wafanyakazi wetu tu, ila kampuni inazingatia zaidi ushauri na maoni ya watumiaji ili kuwapatia kilichobora zaidi ukilinganisha na zilizopita”.

“Na katika kuhakikisha tunaenda na wakati TECNO imewaletea ‘FACE ID’ aina mpya ya (security) inayomuezesha mtumiaji kufungua simu kupitia paji la uso ambayo ni tofauti na alama za vidole (fingerprint) kama ilivyozoeleka”. Na kwa kuwapatia wepesi wa kufanya kazi kwa haraka zaidi CAMON X ina wigo mpana  wa kioo chenye nchi 6.0 na uwiano wa 18:9kinachompatia mtumiaji wepesi kugawa kioo na kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja. Alimaliza  

CAMON X inampa mtumiaji uhuru wa kuperuzi na kuangalia video muda wowote pasipo na hofu ya kuishiwa chaji kwani uwezo wake wa betri ni 3750mAh iliyo na kasi ya mtandao wa 4G namemori ya 16GB ROM + 3GB RAM.

CAMON zilitambulishwa pamoja CAMON X pro, ambayo ni tolea pacha kwa kudokezea baadhi ya sifa zake hasa upande wa kamera, ikiwa ni simu ya kwanza duniani kuwa na megapixel 24 mbele huku kamera yake ya nyumba ni sawa na ya CAMON CX yenye 16MP.CAMON X pro inauwezo mkubwa wa kuprosesi vitu kwa haraka zaidi ukilinganisha na toleo lolote la CAMON kwani prosesa yake ni 2.0ghz octa-core na memori ya 64GB ROM + 4GB RAM lakini simu iyo bado haijaingia sokoni rasmi.

Katika uzyaduzi  huo TECNO Tanzania, iliwakilishwa na  wasanii pamoja na waandishi wa habari kutoka vyomba mbalimbali vya Tanzania, msanii Rosary Iwole maarufu kama “ Rosa Ree” na wengineo walipata nafasi ya kushuhudia utambulishwaji wa simu hizi katika soko la dunia nchini Nigeria katika jiji la Lagos kwa mara ya kwanza.
TECNO Tanzania inatoa fursa kwa wateja wa awali wanaweza kutoa (pre order) kuanzia tarehe 13/4/2018.

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.tz.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad