HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 12 April 2018

SHULE YA FOURTAIN GATE KINARA MATOKEO DARASA LA SABA 2017 MANISPAA YA ILALA


Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
SHULE ya Fourtain Gate iliyopo Tabata Segerea jijini  Dar es Salaam imeshika nafasi ya kwanza katika shule 10 bora zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2017.

Wakati Shule ya Msingi Mtendeni imeshika nafasi ya kwanza kwa shule bora za Serikali ambapo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo imetoa tuzo kwa shule hizo pamoja na nyingine ambazo nazo zimefanya vizuri.

Akizungumza Dar es Salaam leo baada ya kukabidhiwa tuzo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema , Mwalimu Mkuu wa Shule ya Fourtain Gate Julius Luge amesema shule yao imefanya vizuri kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya menejimenti, walimu, wanafunzi na wazazi.

Amesema tuzo hiyo imewapa ari zaidi ya kuendelea kujikita kutoa elimu bura na sahihi kwa wanafunzi wa shuleni kwao na kufafanua mbali ya kufanya vizuri kitaaluma pia wanafunzi wao wamefanya vizuri katika eneo la vipaji,"Moja ya mikakati ya shule yetu ni kufanya vizuri katika eneo la taaluma ya elimu lakini pia tumejikita katika kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wetu .Hivyo tupo vizuri katika taaluma na kukuza vipaji na imani yetu tutaendelea kufanya vizuri zaidi ya hapa,"amesema Mwalimu Luge.

Shule ya Fourtain Gate imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana namna ambavyo imejikita katika kutoa elimu bora na kuhakikisha wanashika nafasi za kwanza kwenye matokeo ya kitaifa na hiyo inatokana na kazi kubwa inayofanywa na walimu katika kuandaa wanafunzi wao kitaaluma.Awali Ofisa Elimu Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas akitaja shule zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mbali na Fourtain Gate kwa shule za binafsi nafasi ya pili ni Tusiime, ya tatu St.Joseph Millleniam, nafasi ya nne Genius King, nafasi ya tano Masedonian na sita Lusasaro.

Nafasi ya saba imeshikiliwa na Shule ya Batvalley , nafasi ya nane Nyiwa, nafasi ya tisa Herritage na nafasi ya 10 ni Green Hill.Kwa upande wa shule bora za Serikali Thomas amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Shule ya Msingi Mtendeni,Shule ya Msingi Zanaki imeshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ni Shule ya Msingi Kiwalani.

Ametaja nafasi ya nne ni shule ya msingi Olimpio, nafasi ya tano Shule ya Msimbazi Mseto, nafasi ya sita Shule ya Msingi Diamond, nafasi ya nane Shule ya Msingi Lumumba, nafasi ya tisa Shule ya Msingi Mkoani na nafasi ya 10 Shule ya Msingi Maktaba.Manispaa ya Ilala katika matokeo ya mtihani wa darasa
la saba mwaka jana kimkoa imeshika nafasi ya pili na kitaifa imeshika nafasi ya nne.Hata hivyo shule hizo zimetakiwa kuongeza juhudi ili washike nafasi ya kwanza kwa matokeo ya mwaka huu kwa ngazi ya kitaifa na kimkoa.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Sophia Mjema(mwenye kiremba) akiwa na Mwalim Mkuu wa Shule ya Fourtain Gate iliyopo Tabata Segerea Julius Luge leo baada ya kumkabidhi tuzo maalumu kutokana na shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 10 bora za binafsi katika matokeo ya mtihani wa darasa saba mwaka 2017 kwa shule zilizopo kwenye manispaa hiyo.
 Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza katika hafla za utoaji wa tuzo hizo leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na walimu,wanafunzi katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa shule za msingi zilizofanya vizuri katika Manispaa ya Ilala leo jiji Dar as Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad