MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa
ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya
Mamlaka hiyo kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim.
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza wakati wa
ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya
Mamlaka hiyo kulia Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald
Ngaire kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akizungumza wakati akiwakaribisha
wageni kwenye sherehe hizo zilizofanyika kwenye viwanja v ya Bandari
Jijini Tanga
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akifuatilia
matukio mbalimbali kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
kulia ni Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire.
Afisa
Tehama wa Bandari ya Tanga Ally Isaka akimueleza kitu Mkuu wa wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo
katikati ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
Meneja
wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiteta jambo na Mkuu wa
wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja
vya Bandari leo akiwa ameambatana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga
(OCD) Jumanne Abdallah na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha
Salim.
Sehemu ya wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakimsikiliza Mkuu wa
wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Sehemu ya wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakimsikiliza Mkuu wa
wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Zoezi la utoaji wa damu likiendelea kwenye sherehe hizo
SERIKALI
mkoani Tanga imesema kuwa haitakuwa na simile na wananchi
watakaokamatwa kujihusisha na kuingiza bidhaa za magendo kupitia bandari
bubu kwani wanachangia kuikosesha mapato serikali.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati wa ufunguzi
wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka
hiyo.
Alisema kuwa kumekuwepo na wimbi kubwa la wafanyabiashara
wasio waaminifu kutumia bandari bubu kupitishia bidhaa za magendo ambazo
sio salama kwa matumizi ya binadamu.
“Katika hili hatutakiwa na
msamaha wala kumuonea mtu haya tukikukamata chombo tutakitaifisha
pamoja na mali zake huku muhusika atachukuliwa hatua kali za kisheri
nilazima wananchi wajifunzi kuona umuhimu wa kutumia bandari
rasmi”alisema DC Mwilapwa.
Aidha aliitaka Mamlaka ya usimamizi
wa bandari Mkoani Tanga kuhakikisha utendaji kazi wao unaendana na kasi
ya maboresho ya bandari hiyo unaofanywa na serikali kwa sasa.
Awali
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama alisema kuwa maboresho ya
vifaa na vitendea kazi katika bandari hiyo yameweza kusaidia kuongeza
ufanisi wa kuhudumia shehena za mizigo kutoka siku kumi hadi nne.
Alisema
kuwa kuhudumia shehena za mizigo katika kipindi kifupi kumesaidia
kupunguza gharama kwa wateja wanaohudumiwa na bandari hiyo . “Licha ya
kuhudumia mizigo kwa awamu mbili lakini uwepo wa vifaa umesaidia
kuboresha uwezo wa bandari yetu ya kuhudumia mizigo kwa ufanisi
zaidi”alibainisha Mkuu huyo.
Sherehe hizo zinakwenda
sambamba na kauli mbiu Bandari za TPA ni chachu ya uchumi Viwanda na
Ustawi nchini Tanzania (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga
Raha)
No comments:
Post a Comment