HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 20, 2018

RC MAKONDA AZINDUA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO CHANIKA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
RAIS wa Shirika la Misaada la Korea Kusini (KOICA), Lee Mi Kyung amezindua Hospital ya Mama na Mtoto Chanika iliyojengwa kwa jitihada  za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliyetafuta wafadhili hao.

Ujenzi wa hospital hiyo ya kisasa umegharimu zaidi Sh.billion 9.8 ambapo ndani kuna vyumba vya kisasa vya upasuaji, vyumba vya madaktari, maabara, chumba cha mionzi, wodi ya wazazi,wodi ya watoto njiti na chumba cha operesheni (Theater).

Pia vyumba vya kujifungulia, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), vyoo vya kisasa pamoja na nyumba za familia 28 za madaktari ambapo ndani ya nyumba hizo kuna huduma zote za muhimu.

RC Makonda amesema aliamua kutafuta wafadhili wa kujenga hospital hiyo baada ya kuona kilio cha kinamama waliokuwa wakipoteza maisha na watoto baada ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya. 

Aidha RC Makonda amemuomba Rais wa KOICA kumjengea hospital nyingine mbili kwenye Wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni ili kusaidia maboresho ya huduma za afya. 

Pamoja na hayo Makonda ameshukuru Serikali ya Korea Kusini kwa ufadhili wa hospital hiyo yenye hadhi ya kimataifa.

Kwa upande wa Rais wa KOICA Lee Mi Kyung amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo huku akipongeza Tanzania kwa kudumisha amani tofauti na Mataifa mengine. 

Uzinduzi wa hospitali hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa magari mawili ya kisasa ya kubeba wagonjwa (ambulance).
  Rais wa KOICA bi. Lee kwakushilikiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa hospitali ya Mama na Mtoto Chanika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)
 Rais wa KOICA, Lee Kyung akimkabidhi funguo ya gari la kubeba wagonjwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  jijini Dar es  Salaam.
 Muonekana wa gari la wagonjwa lililokabidhiwa  na Rais wa KOICA 
Rais wa KOICA bi. Lee kyung akisalimiana na baadhi wagonjwa katika hospitali hiyo mara baada ya kuizindua.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Rais wa KOICA bi. Lee Kyung wakiwaaga wananchi walihudhuria uzinduzi wa hospitali hiyo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad