Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Vodacom imeamua kuwaweka
pamoja wateja wake zaidi ya milioni 12 kupitia huduma ya Iflix.
Ambapo Vodacom imeingia mkataba na kampuni ya Iflix inayotoa
huduma ya burudani katika nchi zinazoendelea ambapo huduma
hiyo inawapa wateja wanaotumia mtandao wa Vodacom
kuangalia vipindi bora duniani,sinema na vingine vingi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kuingia
makubaliano hayo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Hashim
Hendi amesema kampuni yao imedhamiria kuingiza Tanzania
katika huduma ya kidigitali hasa kwa wateja wao.
Aidha Hendi amebainisha hata wasanii na waandaaji wa filamu
watapata fursa ya kuuza kazi zao katika kampuni hiyo ambapo
italeta kipato katika tasnia hiyo inayofanya vema hapa nyumbani
na nchi za Afrika Mashariki kwa ujumla.
"Ikiwa imeshasaini zaidi ya kampuni 240 ya usambazaji
duniani,Iflix inawapa watazamaji wake chaguo kubwa la vipindi
vya Tv vinavyosifika pamoja na sinema zinazopendwa na mashabiki
kitaifa ikiambatana na sinema kubwa za Bollywood kama vile
Love Shagun,Sharafat Gayi tel lene na nyingine nyingi,"amesema
Hendi.
Kwa upande wa Muandaaji wa filamu nchini Rita Paulsen
amesema wanayofuraha kwa Iflix kuwatambua waandaaji wa
filamu Tanzania na kuongeza hatua hiyo itasaidia kwenda na
wakati.
Wakati Muanzilishi wa Iflix Britt amesema anayo furaha ya kuingia
ubia na Vodacom kufikisha huduma hiyo nchini Tanzania.
"Tumedhamiria kuwapatia chaguo kubwa kabisa la vipindi vya
burudani kwa uhitaji wa matakwa yao wenyewe waweze kutazama
au kupakua kwenye kifaa chochote atakachopenda
mteja"amesema Britt.
Ili mteja kupata huduma hiyo anatakiwa kupakua App ya Iflix bila
malipo,na vifurushi maalum mteja ata bonyeza *149*01# kisha
kuchagua intanenti halafu kifurushi ikifuatiwa na Iflix,kifurushi cha
siku kwa Sh.1,000,cha wiki 6,500 na cha mwezi 18,000.
Mkurugenzi kitengo cha biashara Vodacom, Hashim Hendi akizungumza katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam mara baada ya makubaliano hayo kuhusu huduma hiyo ya Iflix inavyoweza kutoa burudani kwa wateja wao.
Mkurugenzi mkuu Iflix Britt akizungumza katika ofisi za makao makuu ya Vodacom Jijini Dar es salaam namna na jinsi huduma hiyo katika utendaji wake wa kazi kuonyesha filamu mbalimbali pamoja na vipindi vingine vingi hapa duniani
Mwandaaji wa Filamu nchini Rita Poulsen akitoa shukrani kwa Iflix kwa kuweza kuwatambua waandaji wa Filamu Tanzani na kufikisha huduma hiyo katika ofisi za Vodacom Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment