HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 5, 2018

MUSTAFA HASSANAL AZINDUA MAVAZI YAKE MAPYA NCHINI NIJERIA, AZUNGUMZIA ANAVYOGUSWA NA MATATIZO YA WANAWAKE


 Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MBUNIFU nguli wa mavazi barani Afrika Mustafa Hassanali wiki hii amepata nafasi ya kuwa mmoja kati ya wabunifu 45 kutoka nchi za Afrika , ambao wameshiriki kuonesha mavazi yao ya kipekee katika jukwaa la kifahari la Arise Fashion Week lilofanyika jijini Lagos nchini Nigeria.

 Hassanali aligusa jukwaa la maonyesho hayo Aprili 1 mwaka huu kwa kuzindua mavazi yake aliyoyapa jina la Endometriosis, mavazi yaliyokuwa na nia ya kusambaza ufahamu kuhusu uwepo wa ugonjwa wa endometriosis na kutoa mchango kwa wanawake ambao wametambulika kuwa na ugonjwa huo.

Huku  wakiishi na mapambano ya kufanya matibabu tofauti tofauti iwe, upasuaji, vidonge, na dawa za vimiminika katika kutibu maumivu sugu wanayoishi nayo.

Akizungumza baada ya kupata nafasi hiyo amesemw “Nimekuwa na fahari ya kuingia katika sehemu ya maisha ya mwanamke, sio tu kwa kubuni nguo bali kutengeneza nguo yenye maana inayobeba ujumbe shawishi  kwa jamii.

"Mavazi yangu yenye jina la endometriosis yana nia madhubuti ya kumuunga mkono rafiki yangu Millen Magese ambaye safari yake ya kuishi na endometriosis imekuwa ya kusikitisha na yenye mhemuko wa huzuni, vilevile inaonyesha nguvu ya mwanamke kuwa hata ukipitia maumivu yote hayo, siku zote kuna mwanga na kuleta msukumo kwa wanawake wote dunia”

Amefafanua ni kama methali ya Kiswahili inavyosema, “ukiwa unataka kwenda haraka, nenda  peke yako, ukiwa unataka kwenda mbali nenda pamoja na wenzako”  na hivyo safari ya Mustafa katika ulimwengu wa mitindo ni mfano ulio hai unaoashiria umoja unaopigania matatizo mbalimbali ya wanawake kwenye jamii, iwe ujasiriamali au matatizo ya kiafya.


Amesema kwa miaka 18 iliyopita, Mustafa amekuwa akijitolea kuwa msaada kwa wanawake wanaokumbana na matatizo ya kiafya, huku akiwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na sekta hiyo.


Amekuwa mbele katika kutengeneza kampeni  zenye nia ya kusambaza ufahamu kuhusu  Festula, kansa ya matiti na endometriosis kupitia  majukwaa ya mitindo.

Imeelezwa hakika Mustafa ni mtu wa kipekee sana, na mawazo yake makubwa katika utengenezaji wa nguo zake uleta matokeo ya kuweka saini yake ya kuvutia katika ulimwengu wa mitindo.

Pia  kwa mara nyingine wadau wa mitindo nchini Nigeria wameshuhudia kuwa, kweli Mustafa ni mtu wa mitindo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad