HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 29, 2018

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHINDI WA PILI KATIKA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI



Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba (kulia), akipokea tunzo na cheti kutoka kwa Bw. Eric Shitindi katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya MFuko kushinda nafasi ya pili katika masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani tarehe 28 Aprili katika Uwanja wa Kichangani Iringa.


 NA MWANDISHI WETU, IRINGA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeibuka mshindi wa pili katika masuala ya usalama na afya mahala pa kazi katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila mwaka.

Maadhimisho haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) nchini na kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na maonyesho kutoka kwa wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni leo tarehe 29.

Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ameipongeza WCF kwa ushindi walioupata na kuwasihi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba, amefafanua kuwa moja ya malengo ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kukuza na kuendeleza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi.

Mshomba ametoa ufafanuzi huo leo katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa baada ya kupokea tuzo na cheti cha Mshindi wa pili katika masuala ya afya ya usalama mahala pa kazi.

Aidha, akikabidhi tunzo hiyo kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi ameupongeza Mfuko kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika nyanja tofauti tofauti pamoja na kwamba hauna miaka mingi sana toka uanzishwe. “Tunajivunia sana kuona ya kwamba Mfuko umeweza kulipa fidia stahiki kwa wakati, kitu ambacho kilikuwa changamoto hapo awali” Aidha, pongezi zangu ziwafikie kwa kuanzisha mifumo inayoboresha huduma kwa waajili na waajiliwa wote ikiwemo mifumo ya ki- electroniki inayowazezesha waajili kujisajili, kulipia michango na kufuatilia michango yao.

Mfuko umehitimisha maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi katika Mkoa wa Iringa na unajiandaaa na semina ya wadau itakayofanyika tarehe 30 Aprili na hatimaye kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Tarehe 01 May 2018.

Katikati Bw. Eric Shitindi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya kupokea tunzo na cheti katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika Uwanja wa Kichangani Iringa. (Akishikilia kombe pamoja na Bw. Shitindi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
Bw. Ibrahim Mussa  Afisa Madai Mwandamizi – WCF akimhudumia mteja aliyetembelea banda ya WCF katika maonyesho yaliyofanyika  katika viwanja vya Kichangani Iringa.


 Bw. Masha Mshomba akionyesha tuzo na cheti ambavyo Mfuko umetunukiwa.
  Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Anselim Peter wakiwa ameshika tuzo hiyo huku,  Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.


 Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati), akiwa ameshika tuzo hiyo huku,  Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.




Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Fulgence Sebera, akizungumza

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad