HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 29 April 2018

KIGOMA WAOMBWA KUICHANGIA TIMU YA WANAWAKE YA MKOA HUO ILI IFANYE VEMA

Na Ripota Wetu, Kigoma
WADAU mbalimbali wa maendeleo na soka wameombwa kuiunga mkono timu ya Wanawake wa Mkoa ya Kigoma Sisters ili waweze kuendelea kufanya vema kwenye michuano mbalimbali wanayoshiriki.

Ombi hilo limetolewa leo na moja ya viongozi wa UWT Mkoa wa Kigoma Miriam Ntakisivya pamoja na Kaimu Katibu wa Vijana mkoa huo Adam Kagoma baada ya wao kukabidhi chakula kwa Nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili.

Lengo la chakula hicho ni kuwapa nguvu kwa lengo kuwapa hamasa ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi za ndani na zile watakazocheza nje ya Mkoa Kigoma.

Akizungumza baada ya kukabidhi chakula hicho Ntakisivya amesema ni vema wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakaendelea kuichangia timu hiyo kwani inafanya vizuri na ana uhakika ikisaidiwa itafika mbalimbali kisoka.

"Nitoe ombi watu waendelee kuipambania timu yetu ya Mkoa ambayo kwa sasa inafanya vizuri.Pia nimpongeze Miss Ubungo mwaka 2014 Diana Kato kwa kuguswa na kuchangia kile alichokuwa nacho,"amesema.

Amesema watu watakapoisaidia timu hiyo mbali ya kuwafanya wachezaji na viongozi kuandaa mazingira mazuri ya kimchezo pia itatoa nafasi ya timu hiyo kutatua changamoto ambazo wanakabiliana nazo ambazo nyingine zinatokana na kutokuwa na vyanzo vya kutosha kumaliza yale ambayo wanakabiliana nayo.
 Mwakilishi UWT vijana Mkoa wa Kigoma, Miriam Ntakisivya akikabidhi msaada kwa Capten wa timu ya Kigoma Sisters, Sophia Mwasikili kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake wa Mkoa wa Kigoma.
 Mwakilishi UWT vijana Mkoa wa Kigoma, Miriam Ntakisivya pamoja na Kaimu Katibu wa Vijana moa wa Kigoma, Adam .M. Kagoma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wanawake wa Mkoa ya Kigoma Sisters

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad