HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 4 April 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA

Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Doroth Mwanyika amewaasa maafisa wapya  walioajiriwa katika Wizara yake kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wawapo kazini.

Ameyasema hayo wakati alipokutana na watumishi 59 waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

“Suala la huduma bora katika Taasisi za Serikali limekuwa likisisitizwa sana. Sisi kama watumishi wa Serikali ni lazima tutambue wajibu wetu kwa Umma ambao kimsingi ndio waajiri wetu. Wajibu wetu ni kutoa huduma iliyobora na inayokidhi matarajio ya wateja”. Amesema Mwanyika.

Katibu mkuu huo amewaasa watumishi hao kuzingatia Maadili mema ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma, kutoa Huduma kwa Mteja na Namna ya kushughulikia Malalamiko, Umuhimu wa Utunzaji wa Kumbukumbu.

Aidha, aliwata watumishi hao kuzingatia mafunzo watakayo pata kuhusu namna ya kujikinga na Janga la Ukimwi na Athari zake, Umuhimu wa Kuwajali Wateja na namna ya Kuwahudumia, Maadili ya Utendaji Bora ikiwa ni pamoja na kujiepusha na rushwa kazini.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Doroth Mwanyika akiongea na  watumishi 59 waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 Baadhi ya watumishi waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Katibu Mkuu, Doroth Mwanyika akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wapya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad