HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 22 April 2018

KAOLE SNAKE PARK YAIPIGA TAFU UMISETA NA UMITASHUMITA BAGAMOYO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kaole Snake Park, Kauthar Kihuhe(kushoto) akikabidhi msaada wa Jezi kwa Kaimu Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo, Danny Mporere zenye thamani ya Shilingi milioni moja na laki mbili(1200,000) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika kituo hicho cha utalii wa ndani kilichopo Bagamoyo mwishoni mwa wiki.Kulia ni Afisa Utamaduni Wilaya ya Bagamoyo, Stellah Moshi na Afisa michezo Wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mziba
KITUO cha Utalii wa ndani cha Kaole Snake Park kilichopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani kimetoa msaada wa jezi kwa kambi za Umoja wa Shule za Sekondari Bagamoyo(UMISETA) na Umoja wa Shule za Msingi Bagamoyo(UMITASHUMITA) ambazo ziko kambini zikijiandaa na masindano ya Wilaya kuelekea Mkoa wa Pwani vyote vyenye thamani ya Shilingi milioni moja na laki mbili (1200,000).

Akizungumza wakati wa makabidhiano Mkurugenzi Mtendaji wa Kaole Snake Park, Kauthar Kiguhe alisema Kaule ni wadau wa michezo na kwakutambua thamani ya michezo wamewiwa kutoa msaada huo ili kuleta hamasa kwa vijana waweze kufanya vizuri zaidi tukitambua michezo ni afya, michezo ni kufahamiana lakini michezo hiyo inaweza kuwa ajira kwa vijana hapo baadae mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Alisema Kiguhe, wao kama Kaole wataendelea kusaidia Sekta ya Elimu pale watakapokuwa wananguvu ambapo pia alitoa wito kwa waalimu walipokea msaada huo wawapeleke katika Kituo hicho cha Kaole Snake Park wajue utalii wa ndani unaofanywa na Kaole Snake Park ili wakiulizwa kilichoandikwa kwenye Jezi hozo waweze kuelezea vizuri.
Nae Kaimu Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo, Danny Mporere ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo alishukuru sana msaada huo na kuahidi kuitangaza Kaole Snake Park jinsi inavyjikita katika kutangaza Utalii wa ndani, lakini pia aliahidi kabla ya walengwa wa msaada huo kuanza kuzitumia jezi hizo alisema atawapeleka Wanafunzi kujionea kuifahamu Kaole Snake Park ni nini na inafanya nini.

Mwisho Afisa Michezo wa Wilaya ya Bagamoyo nae alishukuru sana msaada huo kwani umetolewa wakati muafaka timu ziko Kambini kuelekea mashindano ya Wilaya ya kuunda timu ya Wilaya kuelekea Mkoa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad