HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 23, 2018

BENKI YA EXIM YATOA MSAADA HOSPTALI YA RUFAA YA MOROGORO KUPITIA KAMPENI YA “20 YA KUJALI JAMII”

 Hospitali na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa, benki ya Exim Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa imeanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika wodi za wazazi kwenye hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini kama sehemu ya kampeni yake ya mwaka yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.
Benki ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, jijini Morogoro. Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake. 
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ni hospitali ya tisa kupokea mchango huu, baada ya hospitali ya rufaa ya Mwananyamala mwezi uliopita, hospitali  ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mwezi Febuari, hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya mwezi Januari, hospitali ya Mount Meru, Arusha mwezi Desemba, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka jana. 
Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo na mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa Morogoro Dk Lucy Nkya na Mganga mkuu mkoa wa Morogoro Dk Francis Jacob.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu alisema, “Katika kipindi cha miaka 20, benki imetambua umuhimu wa jumuiya zinazozunguka eneo la biashara yetu na ndio maana shughuli za kijamii ni muhimu sana kwa Benki ya Exim. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa katika kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu. Ni kwa hili Benki iliamua kusherehekea miaka 20 kwa kusaidia jamii kwa njia ya kampeni inayoitwa, “miaka 20 ya kujali jamii” kuonyesha jinsi tunavyowashukuru. Benki ya Exim itatoa vitanda na magodoro ya hospitali kwa hospitali nchini kote kila mwezi kwa mwaka mzima”. 
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Dk……..alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya kwa nchini. Aliongezea kwa kusema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii .”
Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Shinyanga, Mtwara, Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Benki ya Exim ilitambuliwa kama benki bora kwa huduma ya wateja binafsi mwaka 2017 na taasisi ya The Banker ya Afrika Mashariki na sasa inasheherekea miaka 20 ya mafanikio, ukuaji na kuwa kiongozi katika kuingia katika masoko mapya barani Afrika. Benki ya Exim ilianzishwa mwaka 1997 na imetanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu katika nchi za Comorro (2007), Djibouti (2010) na Uganda (2016). Benki hii inajivunia kuwa ya kwanza ya Kitanzania kuingia katika masoko ya nje ya nchi. Lengo muhimu kwa benki hiyo ni kutengeneza thamani ya uwekezaji kwa wanahisa wake na kufanikisha ukuaji kupitia utoaji wa huduma za tofauti na zinazomfaa mteja.
Katika kipindi cha miaka 20 ya kuwepo sokoni benki ya Exim imejenga taasisi imara kijiografia, katika bidhaa za kivumbuzi, mahusiano mazuri na wateja na uwezo wake wa kutoa huduma kwa haraka zaidi.
Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu  akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitanda na magodoro 40 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kupitia kampeni yao ya maadhimisho ya miaka 20 ya kujali jamii kwa benki hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya Morogoro, Dk Lucy Nkya akipokea Vitanda na magodoro 40 kutoka kwa Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu, yaliyotolewa na benki ya Exim kupitia kampeni yao ya maadhimisho ya miaka 20 ya benki hiyo yenye kauli mbiu ya "miaka 20 ya kujali jamii".
Mganga mkuu mkoa wa Morogoro, Dk Francis Jacob akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vitanda na mahodoro 40 kutoka benki ya Exim Tanzania kupitia kampeni yao ya maadhimisho ya miaka 20 ya kujali jamii kwa benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad