HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 30, 2018

Benki ya Exim yaendelea kushika nafasi ya tano

BENKI ya Exim imeendelea kubaki katika nafasi ya tano kwa ukubwa ikiwa na rasilimali zenye thamani ya shilingi trilioni 1.6 zitokanazo na ukuaji wa amana kutoka kwa wateja.

Ikiwa ni Benki ya kwanza nchini kufungua Benki tanzu nje ya nchi, Benki ya Exim imeendela kufanya vizuri pia huko ughaibuni. Benki tanzu ya Jibuti ni ya nne kwa ukubwa nchini humo wakati ile ya Komoro ni ya pili visiwani humo. Jibuti ilipata faida ya shillingi billioni 6.5 wakati Komoro walipata faida ya shilingi bilioni 4.8.  Marejesho ya mtaji kwa benki hizo yamekuwa juu zaidi ya kiwango kilichotarajiwa kwa asilimia 50 na 40 kwa Jibuti na Komoro.

Nchini Uganda, ambapo kuna Benki tanzu pia, Benki imeendelea kufanya vizuri na kupunguaza kiwango cha hasara. “Ni mataraji yetu kuwa Uganda itafuata nyayo za Jubuti na Komoro, hivyo kuanza kutengeneza faida kubwa mwaka 2018”, alisema Kaimu Mkurugenzi mkuu, Bwana Selemani Ponda.

Katika mahesabu ya mwaka 2017, faida jumla itokanayo na shughuli za kibiashara nchini Tanzania ziliathirika kidogo kutokana na  mikopo mibaya na pia taratibu mpya za kiuhasibu lenye kuhitaji tengo zaidi kwenye mikopo mibaya. Hata hivyo, matokeo ya kifedha ya biashara mbalimbali katika utendaji nchini Tanzania ukiondoa kuharibika kwa mikopo, Benki imeweza kupata faida ghafi  ya shilingi bilioni 39 kutokana na ongezeko la tengo kwenye mikopo mibaya faida ilishuka mpaka shilingi bilioni 9.6.

“Benki imejivunia kuwa na benki tanzu nje ya nchi, hivyo kuwa na wigo mpana wa kutengeneza faida kutokana na hali nzuri ya uchumi katika nchi husika”, aliongeza kaimu mkurugenzi mkuu, bwana Selemani Ponda.

Exim itafuta mikopo yenye mingine zaidi robo ya kwanza ya mwaka 2018 kufuatana na taratibu mpya za kibenki na kufanya uwiano wa mikopo mibaya kuboreka kutoka asilimia 14.63 mpaka asilimia 8.95. Kaimu mkurugenzi mtendaji bwana Selemani Ponda amethibitisha jitihada za Benki za kuendelea kuboresha ubora wa mikopo kwa lengo la kufikia uwiano wa chini ya asimlimia 5% mpaka mwisho wa mwaka huu.

Mapato yasiyotokana na riba; mapato ya fedha za kigeni pamoja na ada na mapato ya kamisheni yamekua kwa asilimia 24 na asilimia 12 kufikia bilioni 12 na 37 bilioni zilizotokanana kuongezeka kwa miamala katika njia mbalimbali.  "Haya yote yametokana na utendaji mzuri na huduma bora katika mitandao yetu yote,” Mkurugenzi Mkuu huyo alisema.

Kundi la Benki za Exim, ni mojawapo ya benki kubwa nchini ambayo imefanya uwekezaji endelevu katika teknolojia kwa miaka 3 iliyopita. Benki imeanza kuona faida ya uwekezaji huu. Benki imeweza kujijengea nafasi katika nyanja mbalimbali ikiwemo Kampuni kubwa, za kati na ndogo ikiwa imeanzisha huduma hizo za kifedha. Mashine za kuwekea fedha ndani na nje ya matawi, na njia ya kielekronia ya kuwasilisha hundi pasipo kufika tawani zilizovutiwa sana na wateja wa kampuni kubwa unaorahisisha matumizi, uhakiki, uharaka na usalama wa miamala.

Kutokana na ushirikiano mzuri saja kutoka TANAPA (Mamlaka ya Hifadhi za Taifa), Benki ilikuwa waanzilishi wa kwanza katika kuanzisha makusanyo ya katika hifadhi za taifa. Pamoja na benki kutoa huduma ya makusanyo katika hifadhi  za TANAPA nchini kote lakini pia imewezesha upatikanaji wa vibali kupitia mtandao na pia makusanyiko ya ada. 


Kwa mujibu wa kauli mbiu ya Kundi la Benki za Exim, “Exim iko kazini, leo kwa kesho”, Benki imeendelea kutekeleza njia mpya za kukidhi mahitaji ya wateja wa makundi yote wa kampuni kubwa, za kati na ndogo na mteja mmoja mmoja kwa hali ya juu sana.

Mnamo mwaka wa 2017, Benki ilizidi kupanua uwepo wake kama sehemu ya mkakati wake wa kukuza usambazaji huduma za fedha karibu na wateja wake. Benki sasa kwa ujumla ina matawi 46 kwenye mtandao wake; 33 Dar es Salaam, 6 Komoro, 2 huko Jibuti na 5 nchini Uganda. Mbali na matawi yake, Benki ina mashine za fedha -ATM 78, vituo 7 vya huduma ya MoneyGram.

Benki imeadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa tangu kuanzishea Agosti 2017. Kama ishara ya kutoa shukurani kwa wateja wake na jamii, benki imeanzisha mpango wa huduma kwa jamii wa kuchangia vifaa vya hospitali na mradi huu utaendelea kwa mwaka mzima hadi kufikia Julai 2018. “Tunashukuru wateja wetu na jamii kwa ujumla kwa kutuunga mkono, na tunaahidi tutandelea kuboresha huduma zetu kwa ukuaji wa biashara zao na uchumi kwa ujumla”, alimalizao Kaimu Mkurugenzi, Bwana Selemani Ponda.

Benki inategemea kuzindua huduma kadhaa za kidijitali kwa mwaka 2018.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank Tanzania, Selemani Ponda akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu matokeo ya benki ya mwaka 2017. Kushoto kwake ni Kaimu Afisa wa operation David Lusala na Kulia ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Issa Hamisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad