HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 8, 2018

BALOZI KAIRUKI, AZUNGUMZIA MKUTANO JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKUTANO wa  Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na China unatarajia kuanza kufanyika Beijing nchini China.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Remidius Emmanuel kutoka Beijing,China amesema  kesho Aprili mwaka huu saa saba mchana (saa za China ) kutakuwa na mkutano huo.

Lengo mahususi la mkutano ni  kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda  na hasa kwenye viwanda  vya kutengeneza dawa na vifaa tiba. 

Mkutano huu umeandaliwa kwa pamoja kati ya ubalozi wa Tanzania na Taasisi ya maendeleo ya China na Afrika ( China- Africa Development Fund)  ambayo iko chini ya Serikali ya China na ni sehemu ya mwitikio wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk.John Magufuli ya kuona tunavutia uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya dawa ili nchi yetu iweze kuzalisha kwa ajili ya soko la ndani.

"Kwa hiyo tumeitisha mkutano huu na kuna mwitikio mkubwa na kuna kampuni kama 20 ambayo yanatengeneza dawa, kampuni kubwa ya hapa China yameitikia mwaliko, yatashiriki kesho ili kuweza kusikiliza fursa ambazo Tanzania  inazo katika uwekezaji.


"Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu, utaongozwa na mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhammad Bakari ambaye ataambatana na timu ya viongozi wa sekta ya afya wa Tanzania kutoka taasisi za hospitali ya Taifa ya Muhimbili na taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Chuo kikuu cha Afya cha Mhimbili,mwakilishi kutoka taasisi ya MOI (Muhimbili Orthopaedic Institute)

" Vilevile tutakuwepo ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali kwa wawekezaji hao. Ujumbe huu utakuwepo hapa Beijing kuanzia leo hadi Aprili 12 mwaka 2018,"amesema.

Ameongeza kengo lao  ni ifikapo Mei,2018 waandae ziara ya wawekezaji ambao wataonyesha nia sasa yakuja Tanzania kwa ajili ya fursa hiyo ili wakutane na wadau mbalimbali nyumbani nchini Tanzania.

Baadhi ya wadau  ni taasisi  za uwekezaji TIC,EPZA,ZIPA na wengineo pamoja na taasisi ya MSD.

Amesema mbali na mkutano huo wa jukwaa la biashara, watakuwa na ajenda nyingine mahususi  za kujenga ushirikiano kati ya taasisi zao na taasisi za hapa China, matarajio ni kwamba Jumanne ya Aprili  10 mwaka huo ujumbe huu utakutana na na uongozi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Peking cha hapa China.

Amefafanua  Chuo ambacho kinaongoza hapa China na kina hospitali ya kisasa  ambayo inashughulika na magonjwa ya  Ubongo na Mishipa (Neurology) na mazungumzo hayo yanalenga  kubadilishana uzoefu

Pia amesema kutafuta fursa  za mafunzo  ya wataalamu wao katika masuala ya  Ubongo na Mishipa  kama mnavyofahamu Tanzania ina upungufu mkubwa wa  wataalamu hao na wanahitaji kufundisha wataalamu wengi zaidi.

"Pia tunahitaji wataalamu  waje hapa China kupata uzoefu kwa sababu ya ukubwa wa Taifa hili na wingi wa watu, basi wataalamu wa hapa wanao uzoefu mkubwa kwasababu wanashughulika na mambo haya kwa wingi.

"Matarajio yetu kupitia ushirikiano huu utakaoanzishwa baada ya mazungumzo yao na  Hospitali ya  chuo kikuu cha Peking wataalamu kutoka Muhimbili,MOI,Chuo Kikuu Cha Afya Muhimbili wataweza kupata fursa ya kuja kwenye  mafunzo ya muda mfupi, wakati na muda mrefu.

"Hii ni sehemu ya matunda ya ushirikiano ambao Rais  Dk.John Magufuli aliuzungumzia pamoja na ile timu ya wataalamu waliokuja na ile Meli mkoani Dar es Salaam mwaka jana," amesema.

Amefafanu moja ya mazungumzo  Rais aliwaomba watujengee uwezo nao wamekubali ndio maana hiyo timu  itakutana na hao wataalamu wa Chuo Kikuu kuzungumzia  suala la ushirikiano. 

Amesema mbali na masuala ya tiba ya mishipa na ubongo, ujumbe huo wa Tanzania utapata fursa ya kukutana na  taasisi ya saratani ya hapa China inayofahamika kama Chinese Academy of  Medical sciences Cancer Hospital. 
Ambapo taasisi hiyo inayoongoza hapa China  katika masuala ya utafiti na tiba  katika masuala ya saratani, kwa mwaka mmoja inafanya upasuaji wa watu zaidi ya 4,000 katika magonjwa ya saratani za aina mbalimbali.

"Kwa hiyo wana uzoefu mkubwa na taasisi hii na yenyewe pia  wako tayari kushirikiana na Tanzania na Taasisi yetu ya Ocean Road kwa ajili ya kutoa fursa za mafunzo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kufanya utafiti wa Pamoja, tayari tumeanza kuzungumza nao kuangalia uwezekano wa kuanzisha taasisi nyingine ya saratani nchini kwetu kule Dodoma.

"Na Dodoma iko katikati ya Taifa na ndio Makao Makuu ya Serikali, kuwa na Taasisi ya pili ya Saratani pale Dodoma itarahisisha wananchi wanaohitaji  huduma za Matibabu ya Saratani  kwenda Dodoma kwa urahisi kupata tiba hiyo," amesema.

Amesisitiza matarajio yao  Taasisi hiyo ya China itashirikiana na Serikali (Wizara ya Afya) kuangalia namna gani wataanzisha  hiyo taasisi ya pili kwa ajili ya kutoa huduma  bora za saratani kwa  wagonjwa.

Pia amesema ujumbe huo utakutana na Hospitali  bingwa ya masuala ya tiba ya moyo ya hapa China inaitwa “Fuwai Hospital” hao nao wanahitaji ushirikiano na taasisi zetu hasa katika masuala ya utafiti, Mafunzo na masuala ya kubadilishana uzoefu.

" Mnafahamu Serikali imewekeza kwenye sekta ya afya na kwenye tiba ya moyo na matokeo mazuri ambayo yamepatikana  katika kipindi hiki na matarajio yetu ni kwamba tukikuza ushirikiano na  washirika wetu wa China, tutaongeza ujuzi na fusa za wataalamu wetu kupata utaaalamu zaidi,"ameongeza.

Pia na mambo mengine wakayoyafanya , ujumbe huo unatarajiwa kukutana na  uongozi wa wizara ya Afya ya China kuzungumzia kwa ujumla ushirikiano na kupata baraka zao katika maeneo yote hayo.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad