HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 30 April 2018

AZAKI TANO ZA KIRAIA WAPONGEZA RIPOTI YA NANE YA TEITI, WASHAURI FEDHA ZA MADINI ZITUMIKE KULETA MAENDELEO

 Na Said Mwishehe, Blog ya jamii
AZAKI tano kwenye Kamati ya Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia nchini Tanzania(TEITI) zimpongeza Ripoti ya Nane ya taasisi huku wakishauri fedha zinazopatikana kwenye madini zitumike kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kesho.

Kwa mujibu wa Azaki hizo zisizo za kiserikali ambazo ni Publish What You Pay(PWYP-TZ), Gender and Disability , Interfaith base, Trade Union na Corventional NGO,s ambazo si za kiserikali

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu ripoti hiyo ambayo imezinduliwa rasmi na Waziri wa Madini Angella Kairuki, Mjumbe wa TEITI kutoka Azaki hizo za kiraia anayewakilisha Taasisi za kidini, Grace Masalakurangwa amesema baada ya kuzinduliwa kwa ripoti hiyo ni vema ikafikishwa kwa umma.

Ambapo wamefafanua ni vema pia ripoti hiyo ikawekwa kwenye lugha rahisi na nyepesi kueleweka na kwa kufanya hivyo itasaidia watu wengi zaidi na wa makundi mbalimbali kuichambua.

"Tumewaita waandishi wa habari kwa lengo la kuwaelezea namna ambavyo tumefurahishwa na kupongeza  ripoti ya TEITI ambayo imezinduliwa leo. Ombi letu kwao ni vema ripoti hiyo ikawekwa kwenye lugha rahisi ili iweze kuchambuliwa," amesema Masalakurangwa kwa niaba ya azaki hizo ambazo zimesisitiza uzinduzi ni jambo moja na wananchi kutoa maoni yao ni hatua nyingine.

Pia ametoa ombi sasa umefika wakati wa Serikali kutunga kanuni kuhusu sekta ya madini ingawa wanatambua sheria ya madini ya mwaka 2015 ipo lakini wanaamini kukiwa na kanuni kutasaidia kwani sheria hiyo inazungumza kwa upana zaidi.

Akifafanua kuhusu fedha ambazo zinapatikana kwenye eneo la madini, mafuta na gesi asilia ni vema Serikali ikahakikisha zinatumika katika kufanya mambo yenye tija kwa kizazi cha sasa na kijacho na kueleza wao ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya TEITI lakini wanayo nafasi ya kuchambua na kutoa maoni yao kuhusu ripoti ambayo imezinduliwa.

Masalakurangwa amefafanua ipo haja kwa anayekaimu nafasi Uenyekiti wa TEITI kuidhinishwa rasmi toafuti na alivyo sasa kwani bado anakaimu lakini wanaamini akiwa mwenyekiti kamili itasaidia katika kuendesha shughuli zao.

Pia amesema umefika wakati kwa Azaki hizo kwa kila moja kupewa elimu kuhusu TEITI ambapo nao wataipeleka kwa jamii ili kujenga uelewa wa kazi zinazofanywa na taasisi.

Azaki hizo zimeshauri kuwe na utaratibu wa umma kuelezwa mapema kabla ya ripoti kuzinduliwa kwani itatoa nafasi ya kufuatilia hatua kwa hatua na itakuwa njia nyingine ya kuifanya jamii kutambua majukumu ya TEITI.

MWAKILISHI PWYP-TZ ATOA LA MOYONI
Wakati huohuo Mjumbe mwingine kutoka PWYP-TZ Petro Ahham ametoa ya moyoni kuhusu kuhusu ushiriki wa Azaki hiyo kwenye vikao vya TEITI.

"Binafsi kwanza nimetoa maoni yangu kuhusu tatizo la ushiriki wa mjumbe wa PWYP-TZ ambayo iko ngazi mbili.Mosi ni ya kisheria kutoa Tangazo kwenye gazeti la Serikali (hilo tayari kwenye waraka kupitia vyombo vya habari au kwa waziri mwenye dhamana).

" Pili,ni la kijamii"Legitimacy" na utawala na hata kama mjumbe wa PWYP-Tz hajatangazwa kwenye gazeti bado anabaki na uhali kwa jamii ya AZAKI anazoziwakilisha.

"Hivyo kama baadhi ya wajumbe wengine,kwa sababu yoyote ile hawakutangazwa lakini wameendelea kualikwa na kushiriki vikao vya TEITI-Kiutawala-Kwa nini huyo wa PWYP-TZ analengwa? Kwa kigezo gani na taratibu zipi?"Amehoji.

Kutokana na hali hiyo amesema ipo haja ya jambo hilo kupatiwa ufumbuzi wake na amekuwa akifuatilia ili kupata ufumbuzi wake lakini imekuwa kimya na kueleza huenda kuna ajenda inafanyika ambayo haina nia njema lakini ni matumaini yake mambo yatakaa sawa na kuondoa hali hiyo.
 Mjumbe wa TEIT kutoka Asasi za Kiraia anayewakilisha Taasisi za Kidini, Grace Masalakurangwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti iliyozinduliwa na  Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo Jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe kutoka PWYP-TZ, Petro Ahham akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwajibikaji wa serikali kwenye rasilimali za Tanzania ili kuwanufaisha wazawa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad