HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 21, 2018

TTCL,TIGO WAINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA KURAHISHA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WATEJA WAO


Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania(TTCL), limeingia makubaliano ya kibiashara na Kampuni ya Simu za mkononi TIGO yatakayowawezesha wateja wa taasisi hizo mbili kutumia huduma za kifedha kupitia mitandao hiyo miwili kwa gharama zinazofanana.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza ushirikiano wao, Mkuu wa Huduma za TTCL Pesa, Moses Alphonce amesema, TTCL wanaamini ushirikiano huo ni moja ya suluhisho sahihi la mahitaji ya fedha  kwa mtandao ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kusogeza Huduma muhimu kwa wananchi.

"Tumedhamiria kubadili mifumo ya malipo kwa umma na binafsi, tunataka yafanyike kupitia mitandao ili kuongeza usalama na shughuli za kuichumi na Jamii", amesema Alphonce.

Amesema, ili kuhakikisha TTCL inatoa Huduma bora na nafuu wamejithatiti kuhakikisha Huduma hiyo inawafikia walengwa kwa haraka  na kwa usalama wa hali ya juu wa fedha za wateja ili wapate thamani halisi ya fedha zao kupitia viwango vya TTCL.

Amesema, hatua ya kuanzisha ushirikiano wa kibiashara na TIGO, ni muendelezo wa TTCL kurejea kwa kishindo katika soko la Huduma za mawasiliano nchini.

Kwa upande wa Mkuu wa kitengo cha uthibiti na ubora wa Tigo pesa, Angelica Pesha, amesema, ushirikiano wa Tigo Pesa na TTCl Pesa utawawezesha wananchi kutuma fedha kutoka fedha kutoka Tigo kwenda TTCCL kwa viwango vile vile kama mtu anayetuma kutoka Tigo kwenda Tigo.

Ameongeza, lengo kubwa la ushirikiano huo ni kufikisha huduma za kifedha kwa watu wengi zaidi ambao Huduma hiyo haijawafikia ikiwa ni moja ya uthibitisho wa kukua kwa Huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad