HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 16 March 2018

TARIME VIJIJINI WAPATA MSHINDI WA BAJAJI

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime Vijijini Ndugu Castor Tindwa amemkabidhi bajaji mpya Ndugu Godfrey Saire mshindi wa promosheni inayojulikana kama Jiongeze na Mpesa, Shinda na SportPesa inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa Tanzania wakishirikiana na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom.

Akizungumza wakati wa makabidhiano Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime vijijini alisema “Binafsi nimefarijika sana kwa maana huu mchezo upo na upo kihalali na kisheria, watu wengi wamenufaika sana kupitia mchezo huu mfano mzuri ni Ndugu Godfrey Saire ambaye amekabidhiwa bajaji yake”

Hili ni jambo zuri na kuhamasisha kwa kampuni kama SportPesa kutushirikisha sisi viongozi wa serikali katika makabidhiano haya, kwani inaona na kutambua mchango wetu katika jamii, napenda kumpongeza sana Godfrey na naamini kupitia hii bajaji itakwenda kubadilisha maisha yake na familia yake kiujumla.Kwa upande wa mshindi Ndugu Godfrey Saire alisema “Nimeshawahi kushinda pesa taslim shilingi laki tano, laki tatu hadi laki moja kwahiyo niseme kupitia SportPesa imeweza kuniendeshea kipato changu kwa kiasi flani’

“Nashukuru sana kwa hii zawadi itaenda itasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye ulipaji wa ada ya watoto wangu na kufanikisha shughuli zingine za kimaisha, baada ya kuchezesha droo nilipigiwa simu na hamisi tambwe ambaye alinipa taarifa juu ya ushindi wangu. Akaunti yangu ya Mpesa huwa natumia kuwalipa mafundi wangu kutokana na shughuli mbali mbali, natuma salio pamoja na kulipia bili mbali mbali.”Ikiwa zimebaki bajaji kumi mpaka kumalizika kwa promosheni hii,

watumiaji wa mtandao wa Vodacom wanahamasishwa kushiriki ili kujishindia bajaji mpya aina ya Tvs King Deluxe. Ili kushiriki kwenye promosheni mteja wa Vodacom anatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa, kuweka ubashiri wake na moja kwa moja ataingia kwenye droo itakayompelekea yeye kushinda bajaji hiyo.


Mshindi wa promosheni ya Jiongeze na Mpesa, Shinda na SportPesa, Godfrey  Saire(aliyekalia Bajaj) baada ya kukabidhiwa bajaji na Mkurugenzi wa Wilaya ya Tarime Vijijini Castor Tindwa. Pembeni ni wawakilishi kutoka Kampuni za Vodacom na SportPesa.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad