HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 16, 2018

RC TABORA: FICHUE RAIA WA KIGENI AMBAO WATAJIANDIKISHA KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA.

NA TIGANYA VINCENT
MKUU  wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka wakazi wa Wilaya ya Urambo kuwa makini kwa kutoa taarifa sahihi wakati wa zoezi la uandikishaji kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa ili watu wasiostahili wasije wakajipenyeza na kupatiwa vitambulisho bila kustahili.

Akizungumza katika Kijiji cha Ussoke Mlimani alisema kuwa wananchi wanatakiwa kufichua watu wote wasio raia ambao wanataka kujiandikisha ili waweze kupata vitambulisho kinyume cha sheria.

Mwanri alisema huku nyuma Urambo katika sehemu ya Ulyankulu ilikuwa Makazi ya wakimbikizi kutoka nchi jirani na kuongeza kuwa upo baadhi yao wakawa wameshajipenyeza katika maeneo mbalimbali mkoani humo bila kufuata taratibu.

Alisema ni jukumu la kila mkazi wa Urambo ambaye ni mzalendo kufichua mbinu chafu kama zitaka kufanyika ili kuficha ukweli wa mtu kwa makusudio ya kutaka kumpa kitambulisho mgeni.

Mwanri alisema ili zoezi hilo liwe na tija kwao na Taifa ni vema wananchi wakatoa ushirikiano kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), viongozi wa Wilaya wanapomtilia shaka mtu anayetaka kujiandikisha ili uchunguzi ufanyike kuzuia udanganyifu huo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa Wakazi wote wa Mkoa huo ambao wana sifa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenda katika maeneo yalipopangwa ili kujiandikisha kabla ya muda wa mwisho wa zoezi hilo.

Alisema kitendo cha baadhi ya watu kupenda kujiandikisha siku za mwisho kimekuwa kikisababisha msongamano na usumbufu kwa wananchi na kuongeza ili kuepuka ili waende mapema vituoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad