HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 8 March 2018

SPORTPESA KUWAFUTA MACHOZI WASHINDI WA TIKETI

Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa imekabidhi kiasi cha TZS 12,000,000/= kwa washindi 12 wa promosheni za Zali la Mwanaspoti na Shinda na SportPesa. Washindi hawa 12 walijishindia tiketi za kwenda nchini Uingereza kushuhudia mechi ya Ligi Kuu nchini humo kupitia promosheni za Zali la Mwanaspoti na Shinda na SportPesa lakini kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kusafiri hivyo kila mmoja wao kukabidhiwa TZS 1,000,000/= kama fidia ya safari hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti, SportPesa Tanzania Ndugu Tarimba Abbas alisema “Kampuni yetu ina ushirika na klabu mbalimbali ambapo endapo mshindi atapata nafasi ya kwenda kushuhudia mechi atapata nafasi ya kutembelea makao makuu ya klabu hizo ikiwemo Arsenal na Everton.
Kutokana na vigezo na masharti vya promosheni hizi mbili, hatutawaacha washindi wetu mikono mitupu bali kila mmoja wao ataondoka na kiasi cha shilingi milioni moja ambazo watazitumia wapendavyo, na hii ni kwa mujibu wa masharti ya promotion hizo.” Nae Ndugu Musa Yohana Tupa kwa niaba ya washindi wengine alisema
Kwanza kabisa napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya SportPesa, Mimi ni mshindi niliyepatikana kupitia promosheni ya Shinda na SportPesa. “Kutokana na shughuli zangu binafsi niliomba kutosafiri hivyo kuitaka kampuni inilipe fedha badala ya safari kama kanuni na masharti ya promosheni yanavyoelekeza.
Naye Meneja Masoko wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited Bi. Sarah Munema kupitia promosheni yao ya Zali la Mwanaspoti alisema “Napenda kushukuru SportPesa wakiongozwa na Mkurugenzi kwa kujitolea na kuunga mkono promosheni yetu mpaka ilipofikia ukingoni na mpaka hatua hii amabapo tunaenda kuwakabidhi washindi hundi ya shilingi milioni 12.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad