HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 20, 2018

SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA WATAIFA WA UBORESHAJI WA HUDUMA YA UPASUAJI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI ya kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  imezindua mpango wa taifa wa kuboresha huduma upasuaji ambayo kila mtu anaweza kumudu  kufikia 2025.

Akizungumza wakati wa uzinduaji wa mpango huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa mpango huo umekuja wakati mwafaka kutokana na sera ya afya miaka mitano kuisha hivyo mpango huo kuingia katika sera ya miaka mitano.

Dk. Mpoki amesema kuwa mpango huo uko katika muda mwafaka kutokana na hatua mbalimbali za uboreshaji afya kwa wananchi katika upatikaji wa huduma za upasuaji hali ambayo itaokoa maisha pamoja na kuongeza uzalishaji.

“Upasuaji salama ni ishara ya  kila mtanzania anaweza kupata huduma za afya na kuongeza uzalishaji  ,kuboresha huduma za upasuaji bora pamoja na dawa za usingizi ni muendelezo wa kuboresha afya ya uzazi kwa nchi nzima” amesema Dk.Mpoki.

Amesema Tanzania ni nchi ya tatu duniani ambayo imejizatiti katika  utoaji  wa huduma za upasuaji endelevu na kuingiza katika mpango wa taifa  wa upasuaji pamoja watalaam wa dawa za usingizi.

Amesema kuwa serikali itasomesha madakitari  pamoja na wataalam wa dawa  usingizi ili kuweza katoa huduma bora za upasuaji kwa kiwango kikubwa kulingana na wahitaji wa upasuaji.

Aidha amesema mpango utakuwa na tija kutokana na wizara ilivyojipanga katika kushughulikia changmoto za afya kwa wananchi katika kuweza kutoa huduma bora za afya katika pande zote.

Nae Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasioambukiza, Dk. Sarah Maongezi amesema kwa moja ya jarida linaonyesha Tanzania kiwango cha upasuaji kidogo katika mpango uliozinduliwa  kiwango hicho kitapanda.

Dk.Maongezi amesema kuwa watu wanapata matatizo katika upasuaji hivyo mpango wa taifa utakuwa suluhisho kutokana kusomesha wataalam wa upasuaji pamoja na wataalam wa dawa za usingizi.

Amesema kila mtu akifanya katika nafasi yake tutaokoa wanawake kupata uzazi salama katika upasuaji kwa hospitali zote zilizopo nchini.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la GE, Asha Varghese amesema Tanzania imejipanga katika utaoaji wa huduma ya upasuaji kwa kuingiza katika mpango wa taifa.

Amesema kuwa viongozi wa Tanzania wako imara katika kuboresha huduma za afya ikilinganishwa na nchi nyingine.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa taifa wa huduma ya upasuaji, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Shirika la GE, Asha Varghese akizungumza kuhusiana na Tanzania kupokea mpango wa upasuaji na kuingiza katika mpango wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasioambukiza, Dk. Sarah Maongezi akizungumza hali ya upasuaji nchini, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akikata utepe kuashiria uzinduzi mpango wa taifa kuboresha huduma za upasuaji, jijini Dar es Salaam.
Sehemu wataalam wa afya  wa nchi mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa afya unaofanyika nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad