KAMATI ya kitaifa inayoendesha mradi wa pamoja kati ya mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa (UNESCO, UN Women na UNFPA) na serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na wizara nyingine ambazo zinahusika na maswala ya Elimu hususani TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maedeleo ya Jamii, Jinsia, Watu Wazima na Watoto na Wizara ya Sheria na Katiba pamoja na mfadhili wa mradi KOICA imekutana kwa mara yake ya kwanza kujadili mwelekeo wa mradi unawo husu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu.
Mkutano huo uliokuwa chini ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo uliangalia na kubadilishana mawazo ya hatua zilizofikiwa katika mradi huo ulioanza mwaka 2016 na kutekelezwa katika wilaya nne nchini Tanzania (Kasulu, Ngorongoro, Sengerema na Mkoani, Pemba) kwenye kata 22 na kupitia mpango wa mwaka 2018.
Akizungumza kabla ya kusimamia mazungumzo, Dk Akwilapo aliwashukuru wafadhili na pia wadau wengine waliojipanga kufanikisha mradi huo muhimu kwa maendeleo ya wanawake nchini Tanzania na uchumi kwa ujumla.
“Mradi huu ni muhimu sana kwetu, kwa kuwa unachangia juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) na wizara nyingine zinazofanyakazi kwa pamoja bila kuchoka kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu zikiwemo Wizara za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu na Wizara ya Katiba na Sheria MoCLA” alisema.
Alisema wizara hizo zimekuwa zikifanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba taifa linatoa elimu yenye ubora na kusaidia wale waliopo pembezoni wanapata elimu hasa wasichana na wanawake vijana ambao hawako shuleni kwa sababu mbalimbali.
Aliongeza kwamba uwepo wa kamati hiyo na mikutano yake ni matokeo ya makubaliano yaliyoanzisha programu hiyo ya kusaidia wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, ambapo pia kuna kamati ya ufundi inayotangulia mkutano wa kamati ya kitaifa.
Kamati ya ufundi ilikutana Februari Mosi mwaka huu katika ofisi za Unesco, Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, nia ya mkutano wa kamati ni kuhakikisha kwamba mradi huo kwa kushirikiana na wizara husika unatekelezwa katika ubora unaotakiwa.
Aidha aliwataka wadau waliohudhuria mkutano huo wakiwemo wajumbe kutoka serikali ya mapinduzi Zanzibar kuhakikisha kwamba wanaangalia utekelezaji wa mradi huo kwa makini kwa manufaa ya umma wa Tanzania.
Aliwataka wadau waelewe kama mradi huo ni wakwao ili kupatikane mafanikio yanayotarajiwa.
Aidha alisema kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kuboresha sera za elimu kwa lengo la kuifanya elimu inayotolewa kuwa bora zaidi.
Alisema serikali inaelewa vikwazo vinavyowaondoa wasichana shuleni ikiwamo mihemko ya ujana na utamaduni wa baadhi ya maeneo na kusema juhudi lazima zifanyike kuhakikisha kwamba hali hiyo haiendelei kuwapo na wale walioshindwa wanaendelezwa kwa namna nyingine.
Alisema ipo haja ya kuwezesha mazingira rafiki ya usomaji kwa watoto wa kike kwa kuweka tabia chanya miongoni mwa walimu na wazazi kuhusiana na malezi ya watoto wa kike.
Alisema serikali inataka kupunguza mdondoko wa wananfunzi na pia kuwasaidia waliopata bahati mbaya hiyo na kujikuta nje ya mfumo rasmi wa elimu.
Pia iliongeza kuwa serikali inatambua juhudi zinazofanywa na wadau wa maendeleo kama UNESCO, UN Women, UNFPA na KOICA, na kusema itaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa lengo la kuboresha hali ya wasichana na wanawake vijana.
Naye mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kubaisa alisema kwamba mkutano huo wa mashauriano kwa mradi huo unaoendeshwa Ngorongoro, Mkoani Pemba, Kasulu na Sengerema ni muhimu kwa kuwa unapanga mpango kazi na kuangalia namna bora ya utekelezaji wa mradi huo.
Viola akizungumza kwa niaba ya Anne Theresa Ndog-Jatta, alisema kwamba baada ya kukamilika kwa kampeni dhidi ya ukeketaji katika wilaya ya Ngorongoro mwaka jana katika kutekeleza lengo la maendeleo endelevu ya dunia namba 4.7; na utengenezaji wa kitini cha kufunzia walio nje ya mfumo rasmi wa masomo (kazi inayofanywa na UNFPA na Ofisi ya Waziri Mkuu) kunasaidia kuwapo kwa msingi thabiti wa kusaidia wasichana na wanawake vijana kufikia ndoto zao.
Pia mambo mengine yanayokwenda sanjari na mradi huo ni mahusiano kati ya UN Women na Wizara ya Katiba na Sheria ambapo masuala ya sheria zinazokandamiza wanawake yanashughulikiwa.
Naye Kaimu Mkuu wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo alisema kwa mujibu wa utekelezaji wa mradi huo wa kusaidia wasichana na wanawake vijana, kamati hiyo ni ngazi ya juu ya maamuzi ya utekelezaji wa mradi huo na kazi yake kubwa ni kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na malengo yake yanafanikiwa.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kuhaisa
(kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou mara baada ya kuwasili kwenye
mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa
unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana
kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam.
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo (kulia) na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou kwa
pamoja wakipitia ratiba ya mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na
Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na
wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa
(UNESCO) nchini, Jennifer Kotta akitoa neno la ukaribisho na
kutambulisha meza kuu wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na
Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na
wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou, mgeni rasmi Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo, Kaimu Mkuu
wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa
KOICA nchini, Joonsung Park.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard
Akwilapo akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN
na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana
na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi wa KOICA nchini, Joonsung Park ambao ndio wafadhili wa mradi huo
akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya
mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake
vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar
es Salaam.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kuhaisa
akizungumza kwa niaba ya Anne Theresa Ndog-Jatta wakati wa mkutano wa
Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA
wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika
Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou
akitoa salamu za UN WOMEN katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo
kwa mwaka 2018 unaohusu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia
elimu unaofadhiliwa na KOICA uliofanyika katika Hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo akizungumza jambo kabla ya
kumkaribisha mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika
Mashariki, Viola Kubaisa (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Kamati ya
Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa
kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika
Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo (katikati)
na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women)
Hodan Addou (kushoto).
Ofisa
Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa
(UNESCO) nchini, Jennifer Kotta akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa
mradi kwa mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na
Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na
wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Programu anayeshughulikia masuala ya Afya ya Uzazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Fatina Kiluvia akishiriki katika
mkutano wa kujadili utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2018 unaohusu
kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu unaofadhiliwa na
KOICA ambao umefanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam
Afisa
Programu anayeshughulikia Utawala wa Kidemokrasia wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Wanawake (UN Women), Rachael Boma akichangia jambo wakati
wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa
unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana
kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi wa KOICA nchini, Joonsung Park akiuliza swali baada ya wasilisho
la Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa
Mataifa (UNESCO) nchini, Jennifer Kotta wakati wa mkutano wa Kamati ya
Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa
kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika
Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kuhaisa
akishiriki mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa
unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana
kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Mafunzo na Maendeleo ya Utalaamu kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Venerose Mtenga akijibu swali katika mkutano
wa kujadili mwelekeo wa mradi unaohusu kumwendeleza msichana na
mwanamke kijana kupitia elimu unaofadhiliwa na KOICA ambao umefanyika
katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
Ofisa
Mdhamini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Salim Sururu
akichangia wakati wa mkutano wa kujadili mwelekeo wa mradi kwa mwaka
2018 unaohusu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu
unaofadhiliwa na KOICA uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.
Picha
juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya
UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza
wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard
Akwilapo katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Kamati ya
Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa
kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika
Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment