HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 16 March 2018

Serikali yapigia chepuo Program ya Via: Jiandalie Ajira

Serikali imesema program ya Via:Jiandalie Ajira ina mchango mkubwa hapa nchini katika kuwajengea vijana ujuzi ambao unawasaidia kujiajiri na kuajiriwa na hiyo ni moja ya harakati za kufikia uchumi wa viwanda na wa kati..

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknilojia, Dkt. Leonard Akwilapo alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akifungua mkutano wa washirika na wadau wa program ya Via: Jiandalie Ajira kuwa program hiyo itasaidia vijana kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri au kuajiriwa na hiyo ni moja ya harakati za kufikia uchumi wa viwanda na wa kati.

 “Sisi katika serikali tunaunga mkono program hii ambayo inatusaidia kutatua tatizo la ajira nchini kwa sababu inawapa fursa vijana kujiajiri na kuajiriwa,” alisema Dkt. Akwilapo.

Program hiyo inatekelezwa na Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Vijana Kibiashara (IYF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya The Mastercard Foundation, Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) na Mamlaka ya ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwasaidia vijana kupata ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali kukabili tatizo la ajira kwa vijana.

Alisema kwamba program hii ina mchango mkubwa sana nchini katika jitihada zake za kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kwahiyo mkutano huu wa siku saba utatoa fursa ya mjadala, uzoefu kwa vijana waliopata mafunzo hayo na kupata nafasi ya kupitia utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa IYF, Bw. William Reese amesema Tanzania kwa sasa inatajwa kama ni moja ya nchi ya kupigiwa mfano katika juhudi zake za kuwandaa vijana kwenye ufundi, stadi za maisha na ujasiriamali katika harakati za kupambana na tatizo la ajira duniani.

Alisema katika program hii wadau wanaangalia ni kwa njia gani wanaweza kusaidia kuanzisha mitaala kwenye shule za sekondari na vyuo jinsi ya kujua mahitaji ya soko hasa katika kipindi cha sayansi na teknolojia.

“Ni mafunzo ambayo yana muandaa kijana ili aweze kupata ujuzi wa aina mbalimbali kutokana na mahitaji ya soko husika na ni muhimu kuipelekea elimu hii kwenye vyuo vyetu vya ufundi na vyuo vikuu ili vijana waweze kuwa na sifa ya kuajiriwa na kujiajiri.

Aliongeza kwamba katika mkutano huo wadau wote pamoja na vijana watapata fursa ya kubadilishana uzoefu kwenye maeneo kadhaa ambayo yana matokeo chanya katika uzalishaji wa ajira kwa vijana hasa ujasiriamali.

Kwa upande wake, Programu Meneja wa The Mastercard Foundation, Bw Koffi Assouan alifafanua kwamba walijikita zaidi katika kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya mafunzo ya ujasiriamali na stadi za maisha katika kuwasaidia vijana kujikwamua kwenye tatizo la ajira.

“Sekta ya umma na binafsi zinahitajika kufanya kazi kwa karibu kuhakikisha vijana wanapata ujuzi ili uwasaidie katika kujiajiri au kuajiriwa na kuondokana na tatizo la ajira,” Na program ya Via: Jiandalie Ajira imejielekeza katika kutatua tatizo la ajira, aliongeza kusema Assouan

 Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi aliyenufaika na program ya Via Jiandalie Ajira,Bi. Amina Msuya alisema program hiyo imemwezesha kuapata ujizi katika VETA na kuwataka vijana wenzake kujiunga na chuo hicho au kupata mafunzo ya ujasiriamali ili kuweza kujiajiri.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Vijana Kibiashara (IYF),Bw. William Reese, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa washirika na wadau wa program ya Via: Jiandalie Ajira. Ambapo program hiyo nchini inatekelezwa na IYF kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya The Mastercard Foundation, wake Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) na Mamlaka ya ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwasaidia vijana kupata ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali kukabili tatizo la ajira kwa vijana.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Vijana Kibiashara (IYF) Bw. William Reese (kulia) akifuatilia mada baada ya kufungua mkutano wa washirika na wadau wa program ya Via: Jiandalie Ajira. Ambapo program hiyo nchini inatekelezwa na IYF kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya The Mastercard Foundation, wake Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) na Mamlaka ya ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwasaidia vijana kupata ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali kukabili tatizo la ajira kwa vijana, (katikati)  ni Mwenyekiti wa Bodi ya TECC, Bi. Beng’i Issa, kushoto  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Bw. Dkt. Bwire Ndazi na wengine ni washiriki wa mkutano huo.
Wadau wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Vijana Kibiashara (IYF) wakifuatilia mada katika mkutano wa washirika na wadau wa program ya Via: Jiandalie Ajira. Ambapo program hiyo nchini inatekelezwa na IYF kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya The Mastercard Foundation, wake Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) na Mamlaka ya ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwasaidia vijana kupata ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali kukabili tatizo la ajira kwa vijana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad