HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 12, 2018

SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA BHARTI AIRTEL INAYOMILIKI AIRTEL TANZANIA

 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa  kampuni ya Bharti Bi. Tina Uneken-van de Vreede akiwa ameongozana na mwanasheria mkuu wa kampuni hiyo Bw. Mukesh Bhavnani pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano walipowasili kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa  kampuni ya Bharti Bi. Tina Uneken-van de Vreede (kushoto) akiwa na mwanasheria mkuu wa kampuni hiyo Bw. Mukesh Bhavnani (kushoto kwa waziri) pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (kushoto) walipowasili kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akipeana mikono na mwanasheria mkuu wa kampuni ya Bharti,  Mukesh Bhavnani walipokutana  kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam  
  Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiongozana na mwanasheria mkuu wa kampuni ya Bharti  Bw. Mukesh Bhavnani  pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa  kampuni ya Bharti Bi. Tina Uneken-van de Vreede na  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano  walipokutana  kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam  
 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiongoza ujumbe wa serikali katika mazungumzo na mwanasheria mkuu wa kampuni ya Bharti  Bw. Mukesh Bhavnani  pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa  kampuni hiyo Bi. Tina Uneken-van de Vreede na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano  walipoanza rasmi mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam.
PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad