HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 26, 2018

Rekodi kibao za kuogelea za Taifa zavunjwa

Mashindano ya kuogelea ya kutafuta bingwa wa Taifa yameanza kwa vishindo na waogeleaji mbalimbali wameonyesha uwezo wao mkubwa katika kusaka medali kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimaitaifa ya Tanganyika (IST), Upanga.

Katika siku ya kwanza ambapo waogeleaji 150 kutoka klabu 12 za Tanzania Bara na Zanzibar walishindana katika staili tofauti katika matukio 50, waogeleaji 24 waliweza kuvunja rekodi mbalimbali za Taifa.

Muogeleaji wa kwanza kuvunja rekodi ya Taifa alikuwa Natalia Ladha wa klabu ya Taliss katika freestyle ya mita 100 kwa waogeleaji wenye umri kati ya miaka tisa na 10 kwa kutumia muda wa 1.11.52.
Natalia alivunja rekodi yake aliyoiweka mwaka jana ya 1.12.56 katika staili hiyo hiyo kabla ya kuvunja rekodi ya pili ya mita 100 ya backstroke kwa kutimia muda wa 1.22.75. Mwaka jana alitumia muda wa 1.24.66. Mashindano hayo yamedhaminiwa na AAR, Fina, Taliss, Subway, Sayona, Pepsi, Kaka's barbeque at its finest, international School of Tanganyika,Tanzania Swimming Association (TSA) na  Swiss Air.

Muogeaji klabu ya Braeburn ya Arusha, Ellis Anderson alivunja rekodi mbili  ambazo ni mita 100 katika freestyle na 100m backstroke, wakati Chichi Zengeni wa klabu ya Dar Swim Club (DSC) naye alivunja rekodi tatu, mita 100 freestyle, mita 200 Individual Medley na mita 50 kwa staili ya butterfly.

 Waogeaji wengine waliovunja rekodi katika mashindano hayo ni Natalie Sanford ambaye alivunja rekodi katika mita 100 freestyle kwa waogeaji wenye umri kati ya miaka 13 na 14, na pia mita 50 katika staili ya backstroke.
Katika orodha hiyo ni Sonia Tumiotto ambaye ni muogeleaji wa timu ya Taifa ambaye ataiwakilisha nchi katika mashindano ya Jumuiya ya Madola, Australia, Sonia Tumiotto alivunja rekodi ya mita 100 kwenye staili ya backstroke.

Sonia pia alitwaa medali ya zawadi ya katika mita 100 freestyle,  na vile vile katika mita 50 butterfly na mita 200 freestyle.

Katika orodha ya waogeleaji waliovunja rekodi ya Taifa ni Delvin Barick wa Mwanza ambaye alivunja rekodi ya mita 200 Individual Medley (IM) na mita  50 butterfly, Collins Saliboko wa klabu ya Mis Pirahna ambaye amevunja rekodi tatu (mita 200 (IM), mita 100 backstroke na mita 50 butterfly.

Waogeleaji wa klabu ya DSC, Marin DE Villard alivunja rekodi ya mita 100 backstroke huku Smriti Gokarn ambaye pia kutoka DSC alivunja rekodi ya mita 100 katika staili ya backstroke.

Wengine waliovunja rekodi za taifa na kuweka mpya ni Niamh Baker wa Braeburn aliyevunja rekodi ya mita 100 backstroke, Dennis Mhini (mita 100, backstroke na mita 50 butterfly), Romeo Asubisye Mihaly wa Champion Rise aliyevunja rekodi ya mita 50 butterfly na Khaleed Ladha wa Mwanza aliyevunja rekodi ya mita 200 Individual Medley.

Katika historia ya mchezo wa kuogelea nchini, muogeleaji kutoka nchi ya Ukrain, Christian Shirima alishiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo kupitia klabu ya DSC na kuvunja rekodi ya mita 200 ya Breaststroke.

Chiristian kwa kushirikiana na waogeleaji wengine wa DSC, Chichi, Marin na  Maia Tumiotto walivunja rekodi ya mita 200 kwa staili ya Individual Medley katika relay.

Pia waogeleaji wa klabu ya Mis Piranha, Denis Mhini, Yuki Omori, Collins na  Joseph Sumari walivunja rekodi ya mita 200 ya freestyle katika mita 400.

Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Chama Cha Kuogelea nchini (TSA), Imani Dominic alisema kuwa idadi ya rekodi za Taifa zilizovunjwa zinaonyesha kuwa mchezo huo unapata maendeleo na wanaamini watafanya vyema zaidi katika mashindano ya kimataifa.
“Waogeleaji wameweza kuvunja rekodi mbalimbali, wengine wamevunja rekodi zao za miaka iliyopita na wengine wamevunja za waogeleaji wengine, hii ni uthibitisho tosha kuwa mchezo unapata maendeleo na utafikia katika hatua ya juu kabisa kwa siku zijazo,” alisema Dominic.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad