HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 9 March 2018

Polisi kikosi cha usalama barabarani washirikiana na Airtel katika ukaguzi ya magari.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza juhudi zake za kushirikiana na jeshi la Polisi Tanzania ambapo kwa sasa wameshirikiana na polisi kikosi cha barabarani kuitikia wito uliotolewa na Mkuu wa Kikosi cha Polisi Trafiki kuhahakisha kuwa magari yote yanakanguliwa na kuwekewa stika za usalama barabarani.

Kwenye zoezi hilo ambalo limefanyika kwenye makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, maofisa wa kukangua magari kutoka Kikosi cha barabarani walishirikiana na Kampuni ya Airtel kwenye kukagua magari ya kampuni hiyo pamoja na ya wafanyakazi.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Afisa Uhusiano na Matukio Airtel Tanzania Dagio Kaniki alisema kuwa usalama wa barabarani ni la kila mtu na ndio sababu kampuni ya Airtel imeendeleza ushirikiano wake na Polisi Kikosi cha barabarani kwenye kutimiza wito wa Kamishna wa Trafiki Tanzania la kuhakikisha kila chombo cha moto yakiwemo magari ya biashara, magari binafsi, bajaj pamoja na pikipiki zinakanguliwa na kubandikwa stika za usalama barabarani.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukishirikiana na Polisi kikosi cha barabarani kwenye matukio mengi. Ushirikiano huu umekuwa ni muhimu ili kupunguza ajali. Usalama wa barabarani ni jukumu la kila mtu na ndio sababu Airtel imekuwa mbele kuhakikisha hilo linafanyika, alisema Dagio.

Leo wakaguzi wa magari wameshiriki pamoja na wafanyakazi kukangua magari yao. Natoa shukrani kwa jeshi la polisi kitengo cha trafiki kwani kufika kwao hapa kumeweza kuokoa muda wa wafanyakazi wetu kwenda kufanya ukaguzi. Sisi Airtel tutaendelea kushirikiana na Polisi kuhakikisha elimu ya usalama barabarani linafikia kila mlengwa, aliongeza Dagio.

Dagio alitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa Airtel ya kuitikia wito wa ukaguzi wa magari ili kutimiza wajibu wa kila mtu. ‘Natoa rai pia kwa kile dereva ambaye kwa namna moja au nyingine anakuwa anaandikiwa faini za barabarani. Airtel Money ni suluhisho kwani ni rahisi kutumia kwa ajili ya kulipia gharama hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad