HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 14, 2018

OIF YAELEZEA FURSA ZILIZOPO KWA WATANZANIA WANAOJUA KIFARANSA

Shirikala Kimataifa la La Francophonioe (OIF) ambalo linajumuisha nchi 84 
ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa limesema kwamba ni muhimu kwa 
Watanzania kujifunza lugha ya Kifaransa kwa sababu kuna fursa nyingi 
wanaweza kuzipata kwa kuzungumza lugha hiyo. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Francophonioe  ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25, Balozi wa Ufaransa nchini  Frederic Clavier amesema katika nchi hizo kuna nafasi za kazi nyingi 
ambazo kama Watanzania watajifunza Kifaransa wanaweza kuzipata.

Alisema Tanzania inazungukwa na nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa kama Burundi, Jumhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na hivyo kwa wananchi wa Tanzania hiyo ni fursa ambayo wanaweza kuitumia katika shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.
Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier akizungumza kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25.

"Hapa Tanzania wanazungumza Kiswahili na baadhi ya lugha za nje na hili 
linafungua milango ya ajira ndani ya Tanzania na nje ya nchi kwa 
wanaozungumza Kifaransa na ndiyo maana tunatangaza lugha hii ili watu 
waitumie."

"Tanzania inapakana na nchi nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa hivyo ni  muhimu Kifaransa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu kwa manufaa ya  Watanzania ambao wanatamani kupata nafasi katika nchi zinazozungumza Kifaransa," alisema Clavier.

Aidha, Clavier alizungumzia Wiki ya Francophonioe na kuwataka Watanzania 
kujitokeza kwa wingi katika maonesho mbalimbali yaliyoangaliwa na OIF 
ambayo yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa, Allience Française, 
Century Cinemax ya Oysterbay na Jakaya Kikwete Omnisport Park iliyopo 
Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad